Mgombea Mwenza wa Urais kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiagana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafia, Abdulkarim Shah, mara baada ya kumaliza mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Kilindoni Wilaya ya Mafia Mkoa wa Pwani jana jioni, ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea huyo na Madiwani wa Kata za kisiwa hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio
    wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye
    na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe
    wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na
    awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

    Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia
    ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania
    kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na
    mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu
    kujitokeza kumpeleka mahakamani.

    Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa
    kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga
    kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa
    mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa
    mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni
    moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

    Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa
    anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na
    longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere
    aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni
    nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

    Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na
    Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa
    ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki
    kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika
    kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

    Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na
    tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki
    zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja
    haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala
    usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu,
    wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano.
    Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao . Ee
    mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

    Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya
    Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na
    Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu
    wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi
    350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo
    zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao .

    Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM
    wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini
    kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa
    anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila
    kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

    Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya
    walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa
    mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi?
    Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika
    hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu
    gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata
    hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

    CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili
    harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya
    barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze
    waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka
    vielelezo!

    ReplyDelete
  2. Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio
    wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye
    na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe
    wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na
    awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

    Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia
    ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania
    kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na
    mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu
    kujitokeza kumpeleka mahakamani.

    Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa
    kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga
    kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa
    mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa
    mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni
    moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

    Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa
    anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na
    longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere
    aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni
    nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

    Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na
    Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa
    ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki
    kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika
    kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

    Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na
    tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki
    zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja
    haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala
    usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu,
    wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano.
    Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao . Ee
    mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...