Home
Unlabelled
Jeshi la Polisi Nchini Kenya pamoja na familia zao wafanya ibada ya kumshukuru Mungu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
kuchanganya dini na siasa?
ReplyDeleteaskari wko dini moja tuu?
Hivi kwani askari wote wa kenya ni wakristo? au ya waislamu nayo inakuja ambayo itafanyika msikitini?
ReplyDeleteIGP Mwema Upoooooo! kabla ya kuwalowanisha watu kwa maji ya kuwasha hamasisha askari wako kwa imani zao kuiga mfano wa wenzetu watani wa jadi. Ni wazo zuri kwani haya wao ni binaadamu.
ReplyDeleteAFANDE IGP: Ashkari woote razima waende kanishani bira kujari imani zhao. Ndio hata washiramu. Kuiombea inchi. Kama hutaki acha kazi.
ReplyDeleteASKARI: Rakin afande....
AFANDE IGP: Wote mguuuuu sawaaa. Tuone nani anabisha akiwa mguu sawa. Nimchape taburu au kotimasho ahukumiwe kupigwa risasi mpaka afe.
Naona ukandamizaji hapo, wanyonge wako kimya.
Hizi ni mada wakristo wanatakiwa wakatae dini yao kuchafuliwa na mtu mmoja kuonekana inakandamiza. Sio kusubiri watu walalame ndo ujibu, "lakini Mungu si yuleyule?" Ikiwa ni kweli nendeni tukasalie msikitini basi.
atleast wenzetu viongozi wao wana abudu mungu.
ReplyDeletekikubwa wamemshukuru mungu hilo la dini moja au tatu tuliache, je bongo inawezekana?
ReplyDeleteHizo ni mbinu za kuzugia ili kukwepa kupelekwa ICC si unajua lile sakata la vurugu za uchaguzi bado halijapoa, wanadhani ICC itadanganyika na kuwaona watakatifu..lazima wafungwe mwaka huu
ReplyDeleteInapendeza tena sana kwa watu kama wakenya kuamuamini mungu swali ni kwamba je? wataacha ubaguzi wa makabila, kama wamemjua mungu hata wao wajuane asibaguane.
ReplyDeleteWe anon wa Tue Oct 26, 09:38:00 AM, sijawahi kuona mchovu wa fikra kama wewe.
ReplyDeleteYaani kupuuzia uhuru wa kuabudu we unaona sawa? Ibada gani hiyo sasa ambayo wengine wanasali wengine wanalaani moyoni? Hawawezi hata kusema emeni.
Inatakiwa Mungu aabudiwe kwa haki na kweli siyo chini ya vitisho vya kufutwa kazi.
Sisi Tanzania tunaheshimu uhuru wa kuabudu. Ni nchi ya kisekyula. Tukitaka kufanya sala siku ya mashujaa huita wajeshi wakapiga gwaride na pia viongozi wa dini zote wakafanya sala kwa zamu kwa mujibu wa dini zao. Hili ni somo kwa wakenya na dunia ya kisekyula.
Angalia hata sala ya bungeni, haibagui dini ya mtu wala kupendelea dini ya mtu. Kenya na dunia nzima ya kisekyula wanatakiwa wajifunze hili.
Uhuru wa kuabudu pia unajumuisha uhuru wa kutoabudu. Kama mtu hataki, basi asilazimshwe kwa sababu jinle liko kwenye payroll.
IGP atakuwa amefanya kosa kubwa saana ikiwa kenya si nchi ya kikristo. Hivi angesema waende msigitini watu wangekaa kimya? Ahaa, walichukuwa askari wa dini moja tuu. OK!!!!!!
UJUMBE: dini nyengine hazina shea serikalini. Hii ni nchi ya dini hii.
ReplyDeleteHizi komenti ilitakiwa wakenya wazijibu, wako kimya kwa sababu wanajuwa ni mchemsho.
WARNING!!!!!
ReplyDeleteNAONA KUNA HATARI KUBWA YA JUMUIYA MPYA YA EAC.
SISI BONGO TUMEZOEA AMANI NA USAWA, HALAFU TUNAUNGANA NA WATU HAWA WAMEZOEA UBAGUZI WA DINI NA KABILA.
HOJA ZENU ETI MNATAKA KUWAFUNDISHA USAWA. HAPANA WATATUAMBUKIZA UGONJWA.
MNAONAJE WABONGO?????????????????
Mnaolitamani hili kutokea TZ mlie tu. Nchi yetu siyo ys kidini!!!!!
ReplyDeleteHivi kuna wabongo wanafurahia utumbo huu? Sisi hatuchanganyi D na S.
ReplyDeleteAnonymous wa hapo juu.. ningependa kukujibu. Ni kweli ubaguzi wa makabila upo Kenya lakini lazima tuelewe kwamba wakenya walio wengi wanatambua hilo na wapo katika harakati ya kukabiliana na ubaguzi wa namna hiyo. Je, tujiulizeni ubaguzi wa makabila haupo Tanzania? Je, hamna wazazi Tanzania ambao piga ua wasingependa wanao waolewe au kuoa katika kabila fulani? Ni wazo tu... Tusijipumbaze kwa kusema ubaguzi haupo. Ubaguzi wa aina yoyote ile ni sharti upigwe vita punde inapojitokeza. Kutokubali kwamba ubaguzi haupo ni kufumba macho kwa swala zima la ubaguzi kwa mfano ubaguzi wa kidini, kabila na kadhalika. Ubaguzi wa kikabila ni tatizo zaidi Kenya kuliko Tanzania. Pia tunaweza kusema ubaguzi wa kidini ni tatizo zaidi Tanzania kuliko Kenya. Muhimu ni kupambana na ubaguzi na kutambua kwamba ubaguzi upo. Bila kutambua hilo tutakuwa tunajidanganya.
ReplyDeleteWe anon wa Thu Oct 28, 01:27:00 AM,
ReplyDeleteHuo ubaguzi wa kikabila unaosema upo TZ haumdhuru mtu yeyote. kama watu wanataka kuoana kabila moja ili wakafanye mila zao we inakuhusu nini. Huo ni urafiki tuu.
Ubaguzi tusioutaka ni ule wa kuwanyima watu wa kabila nyingine fursa (ya elimu, ajira, ustawi wa biashara, n.k.). Nani hapa bongo huajiri mtu wa kabila lake? utamkuta magazetini kesho yake!!!
Huo ubaguzi wa dini unaousema bongo hebu toa mfano wake, maana sisi hatuujui! Usituambie eti wanaoana dini moja (huwezi kuchagulia watu rafiki).