Rais Mwai Kibaki akikata keki baada ya kumalizika kwa ibada ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu iliyofanywa jana na askari Polisi wa Kenya pamoja na familia zao katika kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica huku Askofu wa kanisa hilo pamoja na makamanda wa Jeshi hilo wakishuhudia.
Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiongea jambo na makamanda wa Jeshi la Polisi nchini Kenya wakati wa ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanywa jana na askari hao pamoja na familia zao katika kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica.
Kikosi cha Misitu pamoja na familia zao wakiingia katika kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica kwaajili ya kuanza ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanywa jana na askari Polisi na familia zao nchini Kenya.
Katekista pamoja na wahudumu wa kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica wakiwaongoza askari Polisi wa Kenya pamoja na familia zao kuingia kanisani kwaajili ya kuanza ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanywa jana na askari hao .
Rais Mwai Kibaki (wa pili kushoto) akiangalia kwaya ya askari wa Kike na wake za maaskari mara baada ya kumalizika kwa ibada ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu iliyofanywa jana na askari Polisi wa Kenya pamoja na familia zao katika kanisa la Romani Catholic upande wa the holy family Minor Basilica.Picha na Anna Nkinda - Nairobi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. kuchanganya dini na siasa?
    askari wko dini moja tuu?

    ReplyDelete
  2. Hivi kwani askari wote wa kenya ni wakristo? au ya waislamu nayo inakuja ambayo itafanyika msikitini?

    ReplyDelete
  3. IGP Mwema Upoooooo! kabla ya kuwalowanisha watu kwa maji ya kuwasha hamasisha askari wako kwa imani zao kuiga mfano wa wenzetu watani wa jadi. Ni wazo zuri kwani haya wao ni binaadamu.

    ReplyDelete
  4. AFANDE IGP: Ashkari woote razima waende kanishani bira kujari imani zhao. Ndio hata washiramu. Kuiombea inchi. Kama hutaki acha kazi.

    ASKARI: Rakin afande....

    AFANDE IGP: Wote mguuuuu sawaaa. Tuone nani anabisha akiwa mguu sawa. Nimchape taburu au kotimasho ahukumiwe kupigwa risasi mpaka afe.

    Naona ukandamizaji hapo, wanyonge wako kimya.

    Hizi ni mada wakristo wanatakiwa wakatae dini yao kuchafuliwa na mtu mmoja kuonekana inakandamiza. Sio kusubiri watu walalame ndo ujibu, "lakini Mungu si yuleyule?" Ikiwa ni kweli nendeni tukasalie msikitini basi.

    ReplyDelete
  5. atleast wenzetu viongozi wao wana abudu mungu.

    ReplyDelete
  6. kikubwa wamemshukuru mungu hilo la dini moja au tatu tuliache, je bongo inawezekana?

    ReplyDelete
  7. Hizo ni mbinu za kuzugia ili kukwepa kupelekwa ICC si unajua lile sakata la vurugu za uchaguzi bado halijapoa, wanadhani ICC itadanganyika na kuwaona watakatifu..lazima wafungwe mwaka huu

    ReplyDelete
  8. Inapendeza tena sana kwa watu kama wakenya kuamuamini mungu swali ni kwamba je? wataacha ubaguzi wa makabila, kama wamemjua mungu hata wao wajuane asibaguane.

    ReplyDelete
  9. We anon wa Tue Oct 26, 09:38:00 AM, sijawahi kuona mchovu wa fikra kama wewe.

    Yaani kupuuzia uhuru wa kuabudu we unaona sawa? Ibada gani hiyo sasa ambayo wengine wanasali wengine wanalaani moyoni? Hawawezi hata kusema emeni.

    Inatakiwa Mungu aabudiwe kwa haki na kweli siyo chini ya vitisho vya kufutwa kazi.

    Sisi Tanzania tunaheshimu uhuru wa kuabudu. Ni nchi ya kisekyula. Tukitaka kufanya sala siku ya mashujaa huita wajeshi wakapiga gwaride na pia viongozi wa dini zote wakafanya sala kwa zamu kwa mujibu wa dini zao. Hili ni somo kwa wakenya na dunia ya kisekyula.

    Angalia hata sala ya bungeni, haibagui dini ya mtu wala kupendelea dini ya mtu. Kenya na dunia nzima ya kisekyula wanatakiwa wajifunze hili.

    Uhuru wa kuabudu pia unajumuisha uhuru wa kutoabudu. Kama mtu hataki, basi asilazimshwe kwa sababu jinle liko kwenye payroll.

    IGP atakuwa amefanya kosa kubwa saana ikiwa kenya si nchi ya kikristo. Hivi angesema waende msigitini watu wangekaa kimya? Ahaa, walichukuwa askari wa dini moja tuu. OK!!!!!!

    ReplyDelete
  10. UJUMBE: dini nyengine hazina shea serikalini. Hii ni nchi ya dini hii.

    Hizi komenti ilitakiwa wakenya wazijibu, wako kimya kwa sababu wanajuwa ni mchemsho.

    ReplyDelete
  11. WARNING!!!!!

    NAONA KUNA HATARI KUBWA YA JUMUIYA MPYA YA EAC.

    SISI BONGO TUMEZOEA AMANI NA USAWA, HALAFU TUNAUNGANA NA WATU HAWA WAMEZOEA UBAGUZI WA DINI NA KABILA.

    HOJA ZENU ETI MNATAKA KUWAFUNDISHA USAWA. HAPANA WATATUAMBUKIZA UGONJWA.

    MNAONAJE WABONGO?????????????????

    ReplyDelete
  12. Mnaolitamani hili kutokea TZ mlie tu. Nchi yetu siyo ys kidini!!!!!

    ReplyDelete
  13. Hivi kuna wabongo wanafurahia utumbo huu? Sisi hatuchanganyi D na S.

    ReplyDelete
  14. Anonymous wa hapo juu.. ningependa kukujibu. Ni kweli ubaguzi wa makabila upo Kenya lakini lazima tuelewe kwamba wakenya walio wengi wanatambua hilo na wapo katika harakati ya kukabiliana na ubaguzi wa namna hiyo. Je, tujiulizeni ubaguzi wa makabila haupo Tanzania? Je, hamna wazazi Tanzania ambao piga ua wasingependa wanao waolewe au kuoa katika kabila fulani? Ni wazo tu... Tusijipumbaze kwa kusema ubaguzi haupo. Ubaguzi wa aina yoyote ile ni sharti upigwe vita punde inapojitokeza. Kutokubali kwamba ubaguzi haupo ni kufumba macho kwa swala zima la ubaguzi kwa mfano ubaguzi wa kidini, kabila na kadhalika. Ubaguzi wa kikabila ni tatizo zaidi Kenya kuliko Tanzania. Pia tunaweza kusema ubaguzi wa kidini ni tatizo zaidi Tanzania kuliko Kenya. Muhimu ni kupambana na ubaguzi na kutambua kwamba ubaguzi upo. Bila kutambua hilo tutakuwa tunajidanganya.

    ReplyDelete
  15. We anon wa Thu Oct 28, 01:27:00 AM,

    Huo ubaguzi wa kikabila unaosema upo TZ haumdhuru mtu yeyote. kama watu wanataka kuoana kabila moja ili wakafanye mila zao we inakuhusu nini. Huo ni urafiki tuu.

    Ubaguzi tusioutaka ni ule wa kuwanyima watu wa kabila nyingine fursa (ya elimu, ajira, ustawi wa biashara, n.k.). Nani hapa bongo huajiri mtu wa kabila lake? utamkuta magazetini kesho yake!!!

    Huo ubaguzi wa dini unaousema bongo hebu toa mfano wake, maana sisi hatuujui! Usituambie eti wanaoana dini moja (huwezi kuchagulia watu rafiki).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...