Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akizungumza katika fainali za mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika jijini Mwanza hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Ilemela,Ainess Samson akizungumza katika fainali za mashindano ya Mitumbwi yaliyofanyika jijini mwanza hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa mashindano ya Mitumbwi wakichuana vikali huku umati mkubwa ukiwa umezunguka sehemu ya ziwa Victoria kushuhudia fainali hizo.


Mkoa wa Kagera umeibuka na ushindi wa kishindo katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi zilizofanyika jijini Mwanza siku ya Jumamosi tarehe 4 Desemba. Kagera ambayo ilikuwa inawakilishwa na timu tatu za wanaume na mbili za wanawake kama ilivyokuwa mikoa mingine, iliweka rekodi ya kuchukua nafasi ya kwanza kwa wanaume na wanawake pia.

Mtumbwi ulioongoza kwa upande wa wanaume ni ule uliokuwa ukiongozwa na Thobias Kyaichumu – Bukoba, ukifuatiwa na Elisha Jackob – Mwanza, namba tatu ni Ukerewe, namba nne Bukoba na nafasi ya Tano ilienda Mwanza.

Kwa upande wa akina mama, Mtumbwi ulioongozwa na Salome Ernest – Bukoba ndio ulioshika namba moja, ukifuatiwa na Ukerewe, namba tatu Mwanza, namba nne Ukerewe na namba tano Bukoba.

Fainali hizi zilizofanyika katika Mwalo wa Kirumba Mwanza, zilishirikisha jumla ya timu 18 za wanaume na timu 11 za wanawake toka mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na mkoa wa kimichezo wa Ukerewe.

Akiongea kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Kanali Mlengo; aliipongeza bia ya Balimi kwa kuendesha mashindano haya ya Mitumbwi kanda ya ziwa, kwani zaidi ya zawadi zinazotolewa mashindano haya yamesaidia sana kujenga umoja katika kanda ya ziwa.

Nae Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja aliwahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano ya mitumbwi kuwa Bia ya Balimi imeazimia kuyakuza na kuyaboresha zaidi kadri miaka invyokwenda mbele, tumepata mafanikio makubwa sana tangu tuanze mashindano haya miaka 12 iliyopita na ni adhma yetu kuyaboresha zaidi na zaidi, aliongeza Minja.
Zawadi walizopata washindi katika fainali hizo ni kama inavyooneshwa katika jedwali;

Fainali Kuu
Wanaume Wanawake
Mshindi wa kwanza 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 400,000 200,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kwa nini zawadi za wanaume na wanawake zinatofautiana.? wakati mtumbwi ni ule ule na maji ni yale yale? (sina hakika kuhusu umbali)

    ReplyDelete
  2. yani hili nami huwa lanikera sana. tofauti ya nini?kuna wanawake wanakimbiza mitumbwi zaidi ya wanaume, hakukuwa hata na haja ya kupunguza urefu, at all kama walifanya hivyo. nimenotice mara nyingi tu hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...