Mkoa wa Kagera umeibuka na ushindi wa kishindo katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi zilizofanyika jijini Mwanza siku ya Jumamosi tarehe 4 Desemba. Kagera ambayo ilikuwa inawakilishwa na timu tatu za wanaume na mbili za wanawake kama ilivyokuwa mikoa mingine, iliweka rekodi ya kuchukua nafasi ya kwanza kwa wanaume na wanawake pia.
Mtumbwi ulioongoza kwa upande wa wanaume ni ule uliokuwa ukiongozwa na Thobias Kyaichumu – Bukoba, ukifuatiwa na Elisha Jackob – Mwanza, namba tatu ni Ukerewe, namba nne Bukoba na nafasi ya Tano ilienda Mwanza.
Kwa upande wa akina mama, Mtumbwi ulioongozwa na Salome Ernest – Bukoba ndio ulioshika namba moja, ukifuatiwa na Ukerewe, namba tatu Mwanza, namba nne Ukerewe na namba tano Bukoba.
Fainali hizi zilizofanyika katika Mwalo wa Kirumba Mwanza, zilishirikisha jumla ya timu 18 za wanaume na timu 11 za wanawake toka mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Mara na mkoa wa kimichezo wa Ukerewe.
Akiongea kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Kanali Mlengo; aliipongeza bia ya Balimi kwa kuendesha mashindano haya ya Mitumbwi kanda ya ziwa, kwani zaidi ya zawadi zinazotolewa mashindano haya yamesaidia sana kujenga umoja katika kanda ya ziwa.
Nae Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja aliwahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano ya mitumbwi kuwa Bia ya Balimi imeazimia kuyakuza na kuyaboresha zaidi kadri miaka invyokwenda mbele, tumepata mafanikio makubwa sana tangu tuanze mashindano haya miaka 12 iliyopita na ni adhma yetu kuyaboresha zaidi na zaidi, aliongeza Minja.
Zawadi walizopata washindi katika fainali hizo ni kama inavyooneshwa katika jedwali;
Fainali Kuu
Wanaume Wanawake
Mshindi wa kwanza 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 400,000 200,000

Kwa nini zawadi za wanaume na wanawake zinatofautiana.? wakati mtumbwi ni ule ule na maji ni yale yale? (sina hakika kuhusu umbali)
ReplyDeleteyani hili nami huwa lanikera sana. tofauti ya nini?kuna wanawake wanakimbiza mitumbwi zaidi ya wanaume, hakukuwa hata na haja ya kupunguza urefu, at all kama walifanya hivyo. nimenotice mara nyingi tu hili
ReplyDelete