Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Benno Ndullu akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu noti mpya zinazotumika nchini leo jijini Dar es salaam ambapo amesema noti hizo zina ubora na viwango vya kimataifa na kuwataka wananchi wawe makini katika kufuatilia na kuzitambua alama muhimu za noti halali ikiwemo ile ya kutoa rangi pindi inaposuguliwa kwenye karatasi nyeupe. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki (BOT) Bw. Emmanuel Boaz.
Mkurugenzi wa mauzo Ukanda wa Afrika wa kampuni iliyohusika katika mchakato wa kutengeneza na kusambaza noti mpya za Tanzania Cranes Currency ya Sweden Bw. Peter Brown akisugua kwenye karatasi noti za nchi mbalimbali zikiwemo dola za Marekani ambazo zinatoa rangi ikiwa ni moja ya alama ya usalama inayozitofautisha na noti bandia inayopatikana pia kwenye noti mpya za Tanzania na kuwataka watanzania kutokuwa na wasiwasi juu ya ubora wa noti hizo.
Toleo jipya la noti za Tanzania, Marekani na Rwanda ambazo zina ubora na viwango vya kimataifa vinavyokubalika zikionyeshwa mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa mauzo Ukanda wa Afrika wa kampuni iliyohusika katika mchakato wa kutengeneza na kusambaza noti mpya za Tanzania Cranes Currency ya Sweden Bw. Peter Brown akiwaonyesha waandishi wa habari utofauti uliopo wa noti ya zamani ya shilingi elfu kumi na noti mpya leo jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Noti kutoa rangisi alama ya usalama, na kama ni alama ya usalama je! hiyo rangi inavyotoka si pesa inazidi kupauka na kuchuja!?. Ubora ni upi hapo!?. Tunaanza kudanganyana kama watoto wadogo.

    ReplyDelete
  2. hahaha....waosha vinywa muipate hyo

    ReplyDelete
  3. teheeeeeeeeee ukisugua noti ikatoka rangi ndo alama ya usalama? hee makubwa... ngoja nikasugue dola nijioneee... au kiwango hichi cha ubora kipo tanzania tuu? dah jamani kamba zingine...
    ukiangalia hata karatasi iliyotumika duh poor quality... wale wa ten percent mpoo? chukua chako mapema usawa mbovu huu!

    ReplyDelete
  4. huu n huni yan noti itoe ranh ndo ina ubora skweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...