Teksi likiburutwa kuelekea kituoni baada ya kukutwa limepaki ndipo-sipo mtaa wa Azikiwe Avenue jijini Dar leo. Madereva wa teksi zinazopaki mbele ya jengo la Benjamin Mkapa Towers leo wamekuwa katika wakati mgumu baada ya maafande na askari polisi wa usalama barabarani kuwavamia na kuwadai kuwa wamepaki vibaya. Madereva hao wameiambia Globu ya Jamii kwamba wanaonewa kwani magari ya kawaida yakipaki hapo hayaguswi wakati wao wakiwa wanalipa kodi zote za kuendesha teksi na pia ada ya kupaki wanayotozwa na jamaa wa Parking Systems wanaonewa. Wanahoji kulikoni hapo Azikiwe wakati mitaa kama ya Samora Avenue magari yanapaki pande zote mbili za barabara bila shida.

Maafande na wana usalama barabarani wakiwa wamevamia teksi mtaa wa Azikiwe Avenue leo
Gari la break down likifunga teksi barabarani hapo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 27, 2011

    Hicho kirova kinaonekana hakijapasi wala hakina bima!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2011

    wamezidi hao....safi kabisa!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2011

    NONA MAAFANDE NA ROVA ZAO WAMEKOSA KAZI SASA KWASABABU NI WAJASIRIAMALI WAMEIBUKA NA MRADI WA TEKSI. KWELI UJASIRIAMALI NI MAENDELEO. SI UNAJUA KUINGIA BURE KUTOKA PESA.
    POLENI WADAU WA USAFIRI

    ReplyDelete
  4. Kwanza kabisa napenda kuwapongeza walioamua kuchukua hatua kuhusu madereva wanaoamua kuegesha magari popote wanapotaka. Tatizo la foleni za magari Dar-es-Salaam si jambo jipya limekuwa likizungumzwa sana. Sasa kama magari yataachiwa yawekwe popote basi hizi foleni zitazidi. Kuhusu madereva wa Samora au kwingineko kuegesha magari vibaya isiwe sababu ya madereva wa Azikiwe na wao kuiga. Kwa sababu kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe. Kama dereva ameegesha gari vibaya mtaa wa Jamhuri basi wewe uliopo mtaa wa Libya usiige wakati unajua unafanya kosa.

    Hongereni sana Police na wote waliohusika katika kuondoa magari haya yanayowekwa bila mpango kwa kisingizio cha kuwa na vibali.

    Mkimaliza hapo wakikaa vizuri hao madereva na kuelewa kuwa nchi ina sheria basi mtembelee na barabara nyingine hasa hiyo Samora eneo la JM Mall nayo ni balaa kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...