Teksi likiburutwa kuelekea kituoni baada ya kukutwa limepaki ndipo-sipo mtaa wa Azikiwe Avenue jijini Dar leo. Madereva wa teksi zinazopaki mbele ya jengo la Benjamin Mkapa Towers leo wamekuwa katika wakati mgumu baada ya maafande na askari polisi wa usalama barabarani kuwavamia na kuwadai kuwa wamepaki vibaya. Madereva hao wameiambia Globu ya Jamii kwamba wanaonewa kwani magari ya kawaida yakipaki hapo hayaguswi wakati wao wakiwa wanalipa kodi zote za kuendesha teksi na pia ada ya kupaki wanayotozwa na jamaa wa Parking Systems wanaonewa. Wanahoji kulikoni hapo Azikiwe wakati mitaa kama ya Samora Avenue magari yanapaki pande zote mbili za barabara bila shida.
![]() |
Maafande na wana usalama barabarani wakiwa wamevamia teksi mtaa wa Azikiwe Avenue leo |
Gari la break down likifunga teksi barabarani hapo
Hicho kirova kinaonekana hakijapasi wala hakina bima!!
ReplyDeletewamezidi hao....safi kabisa!!!!
ReplyDeleteNONA MAAFANDE NA ROVA ZAO WAMEKOSA KAZI SASA KWASABABU NI WAJASIRIAMALI WAMEIBUKA NA MRADI WA TEKSI. KWELI UJASIRIAMALI NI MAENDELEO. SI UNAJUA KUINGIA BURE KUTOKA PESA.
ReplyDeletePOLENI WADAU WA USAFIRI
Kwanza kabisa napenda kuwapongeza walioamua kuchukua hatua kuhusu madereva wanaoamua kuegesha magari popote wanapotaka. Tatizo la foleni za magari Dar-es-Salaam si jambo jipya limekuwa likizungumzwa sana. Sasa kama magari yataachiwa yawekwe popote basi hizi foleni zitazidi. Kuhusu madereva wa Samora au kwingineko kuegesha magari vibaya isiwe sababu ya madereva wa Azikiwe na wao kuiga. Kwa sababu kila mmoja atabeba mzigo wake mwenyewe. Kama dereva ameegesha gari vibaya mtaa wa Jamhuri basi wewe uliopo mtaa wa Libya usiige wakati unajua unafanya kosa.
ReplyDeleteHongereni sana Police na wote waliohusika katika kuondoa magari haya yanayowekwa bila mpango kwa kisingizio cha kuwa na vibali.
Mkimaliza hapo wakikaa vizuri hao madereva na kuelewa kuwa nchi ina sheria basi mtembelee na barabara nyingine hasa hiyo Samora eneo la JM Mall nayo ni balaa kabisa.