![]() |
Hayati Profesa Mushi |
MAZISHI YA HAYATI PROFESA MUSHI YAMEPANGWA KUFANYIKA SIKU YA JUMATANO, SIO JUMANNE KAMA ILIVYOTANGAZWA AWALI, SHULENI KWAKE (DAR ES SALAAM PRIME HIGH SCHOOL) BUNJU B, DAR.
SIKU HIYO KUTAKUWA NA AWAMU MBILI ZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU.
AWAMU YA KWANZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU ITAKUWA NYUMBANI KWA MAREHEMU VICTORIA (NJIA YA KWENDA HOSPITALI YA KAIRUKI) REGENT ESTATE JIJINI DAR KUANZIA SAA NNE KAMILI ZA ASUBUHI.
AWAMU YA PILI YA KUSALIA NA KUAGA RASMI MWILI WA MAREHEMU ITAKUWA KUANZIA SAA SITA KATIKA UKUMBI WA NKRUMAH HALL CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM. BAADA YA HAPO MSAFARA WA KUELEKEA SHULENI KWAKE BUNJU UTAANZA.
ASANTENI SANA
-SUZAN MZEE
PROFESSOR MUSHI ALIKUWA NI MMOJA KATI YA WACHACHE WA KADA NA UTU WAKE. MSAHURI WA KUTEGEMEA KWA KIZAZI KILICHOPO NA KIJACHO. TAIFA, JAMII, NDUGU NA FAMILIA WAMEPOTEZA HAZINA KUBWA.
ReplyDeleteMUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.
AMANI.
MAINA A. OWINO.
RIP Professor.
ReplyDeleteMUNGU AKUWEKE MAHALI PEMA PEPONI BABA YETU MPENDWA. ULIKUWA NGUZO YA FAMILIA SASA HATUNA TENA MSHAURI KATIKA FAMILIA YETU SISI WANA SAKIME TUTAKUKUMBUKA SANA NA TUTAZIDI KUKUENZI. KWANI SISI TULIKUPENDA SANA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI
ReplyDeleteAMEN
LILIAN MUSHI(MAMA MAUREEN)TEGETA
Namshukuru Mungu kwa ajili ya maisha aliyomjalia Prof, ingawa kuondoka kwake kunaumiza sana lakini kwa mengi aliyofanya yataendelea kukumbukwa. Asante Prof Mushi, kwa lecture zako pale Nkurumah, mahali ambapo utaagwa kwa mara ya mwisho, bado zinanipa mwanga wa kukabiliana na changamoto za maisha. Raha ya Milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani. Amina
ReplyDelete