Vazi limebuniwa na Diana Magessa wa Morogoro ambaye alitumia rasilimali ya kipekee ya bati na ngozi pamoja na nakshi ya shanga na bati za kimaasai. Mbunifu huyu alieleza kuwa vazi hili alilibuni kwa kuangalia mavazi ya wapiganaji wa kale na pia mnyama aina ya “Nungunungu” ambaye hutumia ngozi yake yenye miiba kujihami na maadui. Mrembo Nelly alifurahia vazi lake akisema “Unajua huko ni kama unakwenda vitani, na hii nguo inanipa moyo sana najisikia faraja kubwa kuvaa vazi hili”
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu pre-tapes in her National Costume onstage at Credicard Hall on September 7, 2011. She is preparing to compete in the 2011 MISS UNIVERSE® Competition on September 12 at 9:00 p.m. ET broadcast LIVE on NBC from Credicard Hall in São Paulo, Brazil. Vote your favorite contestant into the semifinals on http://missuniverse.com/ members/contestants. HO/Miss Universe Organization, L.P. LLLP
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu pre-tapes in her National Costume onstage at Credicard Hall on September 7, 2011. She is preparing to compete in the 2011 MISS UNIVERSE® Competition on September 12 at 9:00 p.m. ET broadcast LIVE on NBC from Credicard Hall in São Paulo, Brazil. Vote your favorite contestant into the semifinals on http://missuniverse.com/
Huyu mrembo alibebea wapi hili vazi? Manake naona ni mzigo unaojitegemea peke yake!
ReplyDeleteMrembo ametoka kama yupo holy wood vile
ReplyDeleteVazi la uatamaduni wa wapi hilo? Au ana mizizi ya Kirumi!
ReplyDeletemh hil ni vazi la kikorintho!
ReplyDeletevazi ni zuri na linavutia, ila mbona haliendani na anakotoka mshiriki? manake waweza fikiri katokea huko rumi au kule kwao akina Jumong, kama majaji hawafuatilii vigezo vya asili anakotoka mshiriki, basi naamini litampatia alama za juu, manake ubunifu wa vazi hilo ni wa hali ya juu, tena limebuniwa na Mtanzania mwenzetu kwa kweli anastahili pongezi, zaidi tunamtakia kila la heri mrembo wetu.
ReplyDeletehuu ni utamaduni wa sehemu gani ya tanzania?
ReplyDeleteni ubunifu ndio, lakini naona kuna uwezekano wa kukosolewa kwa kushika hiyo ngao ya gamba la kasa (kobe). ninavyojua kasa ni kati ya viumbe vilivyo-hatarini kupotea. kwa wana mazingira hiyo ni shida!
ReplyDeleteTangu lini hilo likawa vazi la kiutamaduni la Mtanzani? aibuu...
ReplyDeletesisi tunaweza ila tunajisahau sana, sasa hapo ndio kaonyesha Vazi la asili la nchi atokako. sijui lini tutajua maana ya kuchanganua na kuelewa tunachotakiwa kufanya
ReplyDeletehongera bana!!!!!!!!! umependeza sana keep it up, i love it
ReplyDelete