Vazi limebuniwa na Diana Magessa wa Morogoro ambaye alitumia rasilimali ya kipekee ya bati na ngozi pamoja na nakshi ya shanga na bati za kimaasai. Mbunifu huyu alieleza kuwa vazi hili alilibuni kwa kuangalia mavazi ya wapiganaji wa kale na pia mnyama aina ya “Nungunungu” ambaye hutumia ngozi yake yenye miiba kujihami na maadui. Mrembo Nelly alifurahia vazi lake akisema “Unajua huko ni kama unakwenda vitani, na hii nguo inanipa moyo sana najisikia faraja kubwa kuvaa vazi hili”
Miss Universe Tanzania 2011, Nelly Kamwelu pre-tapes in her National Costume onstage at Credicard Hall on September 7, 2011. She is preparing to compete in the 2011 MISS UNIVERSE® Competition on September 12 at 9:00 p.m. ET broadcast LIVE on NBC from Credicard Hall in São Paulo, Brazil. Vote your favorite contestant into the semifinals on http://missuniverse.com/members/contestants. HO/Miss Universe Organization, L.P. LLLP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Huyu mrembo alibebea wapi hili vazi? Manake naona ni mzigo unaojitegemea peke yake!

    ReplyDelete
  2. Mrembo ametoka kama yupo holy wood vile

    ReplyDelete
  3. Vazi la uatamaduni wa wapi hilo? Au ana mizizi ya Kirumi!

    ReplyDelete
  4. mh hil ni vazi la kikorintho!

    ReplyDelete
  5. vazi ni zuri na linavutia, ila mbona haliendani na anakotoka mshiriki? manake waweza fikiri katokea huko rumi au kule kwao akina Jumong, kama majaji hawafuatilii vigezo vya asili anakotoka mshiriki, basi naamini litampatia alama za juu, manake ubunifu wa vazi hilo ni wa hali ya juu, tena limebuniwa na Mtanzania mwenzetu kwa kweli anastahili pongezi, zaidi tunamtakia kila la heri mrembo wetu.

    ReplyDelete
  6. huu ni utamaduni wa sehemu gani ya tanzania?

    ReplyDelete
  7. ni ubunifu ndio, lakini naona kuna uwezekano wa kukosolewa kwa kushika hiyo ngao ya gamba la kasa (kobe). ninavyojua kasa ni kati ya viumbe vilivyo-hatarini kupotea. kwa wana mazingira hiyo ni shida!

    ReplyDelete
  8. Tangu lini hilo likawa vazi la kiutamaduni la Mtanzani? aibuu...

    ReplyDelete
  9. sisi tunaweza ila tunajisahau sana, sasa hapo ndio kaonyesha Vazi la asili la nchi atokako. sijui lini tutajua maana ya kuchanganua na kuelewa tunachotakiwa kufanya

    ReplyDelete
  10. hongera bana!!!!!!!!! umependeza sana keep it up, i love it

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...