Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nundu (kushoto) baada ya kuzindua boti 4 za doria majini leo Sept 16.2011katika bandari ya  Dar es Salaam akiwa na Naibu Wake Mhandisi Athmani Mfutakamba (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Mhandisi Omari Chambo (kulia)Uzinduzi huo ni katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru kwa Wizara ya Uchukuzi
 Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nundu (kushoto) akikata utepe kuzindua boti 4  leo katika bandari ya  Dar es Salaam akiwa na Naibu Wake Mhandisi Athmani Mfutakamba (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara yake Mhandisi Omari Chambo (kulia)Uzinduzi huo ni katika maadhimisho ya miaka50 ya Uhuru kwa Wizara ya Uchukuzi
 Sehemu ya wafanyakazi wa TPA wakiwa katika hafla hiyo
 Hizi ndizo boti  zilizozinduliwa  leo katika Bandari ya Dar es Saalam. Boti kubwa mbili  ni za kuongoza meli  na ndogo ni  kwa ajili ya kuwapeleka mapailot na kufanya doria. Shughuli zote hizi zimefanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika  maadhimisho ya miaka ya uhuru kwa sekta hiyo ya Uchukuzi
 Kweli Wanawake wakiwezeshwa Wanaweza!  Hii ni leo Sept,16,2011 katika Bandari ya Dar es Salaam wakati Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nundu  (hayupo pichani ) alipozindua Boti za doria. Juu pichani  ni mwanamke  pekee Mhandisi  katika Tagi la Nyangumi, Bi.  Maisara Rumani ( katikati)  akiwa na Mhandisi Sifuel Felix (kushoto) pamoja na Mhandisi Nicholus Mfumgomara
 Meneja mawasiliano wa TPA Frakline Mziray (kulia) akiwa na msanii mkongwe wa muziki nchini Mzee Muhidini  Maalim Gurumo zalikuwepo kutoa burudani na bendi yake ya Msondo Ngoma Jazz Band
 Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athmani Mfutakamba (kushoto) akizindua eneo la  ujenzi ,wa kutunzia makontena( GEREZANI CREEK CONTAINER YARD) ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara  leo katika  eneo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania jijini Dar es Salaam. Mwenye suti nyeusi  Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omari Chambo ambapo kulia ni Meneja wa Mawasiliano wa TPA Bw. Franklin Mziray
Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Omari Nyundo (katikati) akizindua huduma kwa mteja kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandar Tanzania leo.  Mkurugenzi Mkuu wawa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania Ephraim Mgawe,(kushoto), kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhandisi Athumani Mfutakamba akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Mhandisi Omari Chambo,Ni katika shamrashamra za  Maadhimisho ya ,miaka 50 ya Uhuru katika sekta ya  Wizara ya Uchukuzi. Picha zote na Mwanakombo Jumaa wa Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hizi boti zimeingia lini maana wakuu wabongo wakishaona ajali ndowanaanza sera zao kama zingikuwepo tangu zamani mbona ajali isingetokea huko pemba yani inatia uchungu kwakweli hajali ishu za wananchi mpaka litoke janga kubwa ndo wanaanza kujishauwa yani bongo kazi kweli2 haya ngoja tuone hizo boti zinazofanya patro

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...