Ankal, salaam.
Ajali za Bodaboda zinazidi kuongezeka na kusababisha madhara makubwa katika jamii. Ajali hii imetokea katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Nduli mjinin Iringa uliopo katika Kijiji cha Nduli. Anayeonekana (mwenye asili ya asia) ni mfanyabiashara Salim Abri (Asas) akiwatazama majeruhi kabla ya kukodi usafiri na kuwapeleka majeruhi wawili. Ajali hiyo ilihusisha bodaboda na mwendesha baiskeli aliyekuwa amepakia ulanzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Salim anajulikana kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali dini, itikadi wala hali ya mtu. Huyu ni mtu wa watu, sijui kwanini hataki kugombea ubunge wa Iringa! Hongera sana Asas.

    ReplyDelete
  2. Nina wasiwasi jamaa aliyekuwa akiendesha baiskeli tayari alikuwa amepata chupa kadhaa kabla hajaanza safari

    ReplyDelete
  3. Jamani hizi ajali za bodaboda zimekuwa nyiingi kupita kiasi.

    Hawa vijana wanaendesha bila ya kuvaa mahelmeti halafu wanaendesha kwa spidi utafikiri wako kwenye mashindano fulani hivi.

    Tafadhali askari waelimisheni na jaribuni kuwatoza faini kubwa watapofanya makosa ili liwe funzo kwao.

    Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

    ReplyDelete
  4. Kweli, kulia kabisa kuna madumu mawili, bila shaka ndiyo yaliyokuwa na ulanzi. Lakini Salim si ana ng'ombe na kiwanda cha maziwa? Ahamasishe watu wanywe maziwa badala ya ulanzi.

    ReplyDelete
  5. ANONYM HAPO JUU, JE UKIWA NA MOYO WA KUSAIDIA JAMII BILA YA KUFUATA DINI YA MTU NDIO SIFA YA KUWA MWANASIASA? YEYE NI MFANYABIASHARA, NA ABAKI MFANYABIASHARA!

    ReplyDelete
  6. jamani muwe mnafikira hata kidogo,sasa wewe anon wa kwanza umefikria kweli kablya ya kuandika? hahahaha...daaa sisi watanzania, halafu wewe utakuwa mdini wewe,tabia mbaya.

    ReplyDelete
  7. Ajali imetokea majeruhi wako kati ya barabara hakuna hata anayejitolea kuwa karibu naye labda kumuweka vizuri kumpunguzia maumivu au kumpa huduma ya kwanza??!!

    Watanzania kweli tumetoka mbali, lakini sikujua tumefikia hapa!

    Mdau, Masaki, DSM.

    ReplyDelete
  8. Tujitahidi kuzidhibiti hizo ajali za bodaboda. Na haina haja ya kutaja mtu na asili yake. Haina lazima. Mara nyingi tukiandika magazeti yetu lazima tuandike asili ya kiasia. Jee hii ina faida yoyote? Si jina lake limeshandikwa?

    ReplyDelete
  9. MNYANYUE BASI!!!!

    ReplyDelete
  10. We mdau kutoka Masaki, kwani ulitaka wakupe na picha ambazo zinaonyesha na huduma ya kwanza, unajuaje kama hajapewa hiyo huduma ya kwanza, pia km kweli unajua 1st Aid hautakiwi kumzunguka kwa karibu mgonjwa anatakiwa kupewa space kwa ajili ya kupata hewa, we kumbe ndo hujui kabisaaaaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...