Ankal, salaam.
Ajali za Bodaboda zinazidi kuongezeka na kusababisha madhara makubwa katika jamii. Ajali hii imetokea katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Nduli mjinin Iringa uliopo katika Kijiji cha Nduli. Anayeonekana (mwenye asili ya asia) ni mfanyabiashara Salim Abri (Asas) akiwatazama majeruhi kabla ya kukodi usafiri na kuwapeleka majeruhi wawili. Ajali hiyo ilihusisha bodaboda na mwendesha baiskeli aliyekuwa amepakia ulanzi.
Salim anajulikana kwa moyo wake wa kusaidia jamii bila kujali dini, itikadi wala hali ya mtu. Huyu ni mtu wa watu, sijui kwanini hataki kugombea ubunge wa Iringa! Hongera sana Asas.
ReplyDeleteNina wasiwasi jamaa aliyekuwa akiendesha baiskeli tayari alikuwa amepata chupa kadhaa kabla hajaanza safari
ReplyDeleteJamani hizi ajali za bodaboda zimekuwa nyiingi kupita kiasi.
ReplyDeleteHawa vijana wanaendesha bila ya kuvaa mahelmeti halafu wanaendesha kwa spidi utafikiri wako kwenye mashindano fulani hivi.
Tafadhali askari waelimisheni na jaribuni kuwatoza faini kubwa watapofanya makosa ili liwe funzo kwao.
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
Kweli, kulia kabisa kuna madumu mawili, bila shaka ndiyo yaliyokuwa na ulanzi. Lakini Salim si ana ng'ombe na kiwanda cha maziwa? Ahamasishe watu wanywe maziwa badala ya ulanzi.
ReplyDeleteANONYM HAPO JUU, JE UKIWA NA MOYO WA KUSAIDIA JAMII BILA YA KUFUATA DINI YA MTU NDIO SIFA YA KUWA MWANASIASA? YEYE NI MFANYABIASHARA, NA ABAKI MFANYABIASHARA!
ReplyDeletejamani muwe mnafikira hata kidogo,sasa wewe anon wa kwanza umefikria kweli kablya ya kuandika? hahahaha...daaa sisi watanzania, halafu wewe utakuwa mdini wewe,tabia mbaya.
ReplyDeleteAjali imetokea majeruhi wako kati ya barabara hakuna hata anayejitolea kuwa karibu naye labda kumuweka vizuri kumpunguzia maumivu au kumpa huduma ya kwanza??!!
ReplyDeleteWatanzania kweli tumetoka mbali, lakini sikujua tumefikia hapa!
Mdau, Masaki, DSM.
Tujitahidi kuzidhibiti hizo ajali za bodaboda. Na haina haja ya kutaja mtu na asili yake. Haina lazima. Mara nyingi tukiandika magazeti yetu lazima tuandike asili ya kiasia. Jee hii ina faida yoyote? Si jina lake limeshandikwa?
ReplyDeleteMNYANYUE BASI!!!!
ReplyDeleteWe mdau kutoka Masaki, kwani ulitaka wakupe na picha ambazo zinaonyesha na huduma ya kwanza, unajuaje kama hajapewa hiyo huduma ya kwanza, pia km kweli unajua 1st Aid hautakiwi kumzunguka kwa karibu mgonjwa anatakiwa kupewa space kwa ajili ya kupata hewa, we kumbe ndo hujui kabisaaaaaaaa
ReplyDelete