Watoto wa shule ya msingi wakisoma magazeti kwenye kibanda cha kuuza Magazeti,eneo la Kivukoni Front,Jijini Dar es Salaam.Picha na Mdau Bashir Nkoromo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2012

    Du, naona hao watoto wanaangalia magazeti ya Utaku tu, kweli tunafika kwa mwendo huu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2012

    Hawaangalii news bali udaku. Inasikitisha sana kwa sababu hayo magazeti yanareport mambo uchafu mtupu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2012

    Mwanzo mzuri kwa vijana kujisomea..Lakini angalia kwa umakini magazeti waliyo-'concentrate' nayo('wenye macho yanayoona vizuri watayatambua) halafu kadiria umri wao,halafu tafakari mwenyewe.Wazazi/walezi kazi tunayo...

    David V

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2012

    watoto wa shule kwa magazeti ya udaku weeeee

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2012

    Nimeipenda sana hii picha>

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2012

    Ni vizuri! Lakini mnaona magazeti wanyotilia mkazo hapo! Ukitaka kujua tunasoma magazeti gani waangalie hao watoto!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2012

    UKIANGALIA KWA MAKINI HIYO PICHA, MACHO YOTE YAPO KWENYE MAGAZETI YA UDAKU (HAPO INA MAANISHA NINI WADAU?)

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 03, 2012

    Hamna cha nyuuzzz wala nini mdau, wewe huoni wamekodolea kwenye udaku tuu? Sijui tunawafundisha watoto wetu nini......

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 03, 2012

    Kinachonisikitisha ni kuwa watoto wote hao macho yao yako kwenye magazeti ya udaku (Uwazi, Sani, Risasi) Tutajenga wababa wenye maadili kweli kwa staili hii???

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 03, 2012

    MBAYA KUONA WATOTO WANASOMA MAGAZETI YA AJABU KAMA UWAZI KIAKILI YANA HARIBU WATOTO UPEO WA FIKRA, WATOTO HAO MACHO YAPO KATIKA MAGAZETI YA UMBEA WA KINAFKI NAKUDANGANYA JAMII. MZ.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 03, 2012

    Kwakweli mimi masikitiko yangu ni habari wanazoziangalia hao watoto. Natamani wangekuwa wanasoma hayo magazeti mengine, lakini wako kwenye habari zinazowabomoa mawazo na wala sio kuwajenga. Wadau tujadili ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia na kuwakinga hawa watoto na huu uhuru wa habari uliopitiliza mipaka. Lets unite and save this unprotected generation.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 03, 2012

    magazeti wanayoyasoma sasa, kaaazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 03, 2012

    Hii ndio picha halisi ya aina ya habari tunazozipa umakini zaidi...ukiangalia kwenye page display hizo gazeti za udaku ndio zimepewa kipaumbele full page display magazeti mengine half page...
    Salma. H

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 04, 2012

    Sina uhakika kama mnaosema kuwa hao watoto wanasoma magazeti ya ajabu mko SAHIHI!! Haiwezekani magazeti ya ajabu yakaanikwa hadharani. Na kama yasingekuwa yanatakiwa kusomwa na watoto, basi sheria ingekuwepo ya kuwalazimisha wauzaji kutokuyapanga kama yanavyoonekana, na badala yake wangewekea bango tu lenye maneno kuwa magazeti ya UWAZI, KIU, RISASI, nk, pia yapo. Basi wale wapenzi wa hayo magazeti wangepatiwa tu. Lakini kama yako wazi hivyo, ni rukhusa kwa kila mmoja. Hakuna haja ya kuwanyanyasa watoto. Serikali ikiona kuwa watoto hawatakiwi kuyasoma, wataweka utaratibu mzuri.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 04, 2012

    There is nothing wrong to read udaku. They are doing this out of "Intellectual curiosity". However, it is society's responsibility to prepare them to become informed consumer of information. GOOD JOB KIDS!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 04, 2012

    Hili ni mojawapo ya mambo yanayoporomosha jamii yetu. Siku hizi ukitembea kila mtaa unaona madanguro,vioski vya pombe,bar,guest bubu,waenda uchi........nk na jamii imekaa kimya inafaudu mambo! Acha vijana nao wapate raha zao kitachotokea baadae nani anajua?

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 04, 2012

    Tuache mawazo mgando! Hayo magazeti watoto walikuta yakiwa yamepangwa tayari! wala hakuna aliyebeba gazeti mkononi ili kutupatia evidence kwamba wanasoma udaku! Sioni kosa lolote la watoto hapo! Watanzania bado kazi ipo!!!

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 04, 2012

    Wanasoma Udaku. Ni taswira ya wazazi na walezi wao. mtoto wa panya ni panya tuuuuu!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 04, 2012

    KAMA WAZAZI WANASOMA UDAKU ,KWANINI MNASHANGAA WATOTO ?HAMNA CHA KUSHANGAZAZA HAPO ............NA KWA TAARIFA YENU HAMNA MAGAZETI YA WATOTO BONGO ,TUMEWANYIMA WATOTO HAKI YAO,HII BUSSINESS IDEA KWA WANAHABARI KUCHANGAMKA KUWA NA MAJARIDA YA WATOTO YENYE KATUNI ,MAFUMBO MICHEZO ,MAZOEZI YA KIELEIMU ETC

    MDAU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...