Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Anselim Peter akitoa pole kwa wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam wakati wafanyakazi wa mfuko huo waliposhiriki futari na wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo. Kushoto ni Meneja Masoko wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina
Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Anselim Peter akiandaa futari kwa mmoja wa wagonjwa hao.
Meneja Masoko wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina akimpa futari mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Anselim Peter akishirikiana na baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kugawa ftari.
Baadhi ya wagonjwa wakipata futari.


Hongereni Mfuko wa GEPF kwa kuwafikiria wagonjwa wa Saratani tumeona Mifuko mingine ikifuturisha Kempisky au Movenpick tena kwa wafanyakazi wenye uwezo. Keep it up
ReplyDeleteHongereni GEPF kwa kufuturisha wagonjwa wa saratani tumeshuhudia mifuko mingine ikifuturisha Kempisky au Movenpick kwa wafanyakazi wao wenye uwezo. Keep it up
ReplyDeleteNawasifu sana GEPF kwa kufuturisha wahitaji halisi, kweli huu ni Mfuko unaoilenga jamii. Hongereni sana, na wengine mfuate sasa !!!!
ReplyDeletebila shaka mmeipeleka futari inapotakiwa
ReplyDeleteAhsanteni GEPF kwa kuijali na kushirikiana na Jamii katika Mfungo wa Ramadhani.
ReplyDeleteGEPF mmefanya jambo jema sana kwa kutoa futari kwa wagonjwa ambao inawezekana sio wafanyakazi wa Mfuko au pia huenda wasiwe wateja wa Mfuko, isipokuwa Mfuko wa PPF sikuwaelewa walipojiandalia futari Wafanyakazi wa Mfuko!!!
ReplyDeleteHivi kweli unaenda kutoa msaada wa futari halafu chakula unapakulia mfuniko wa plastiki? kweli hii si dharau,mmeshindwa kabisa hata kununua vijiko kwa ajili ya kupakulia chakula? mnakudhalilisha na kukitia aibu chombo cha serikali kwa kweli.
ReplyDelete
ReplyDeleteNAWAPONGEZA SANA GEPF KWA KUFUTURISHA WAGONJWA. HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA KUWA SIO KAMA MASHIRKA MENGINE YANAYO FUTIRISHA MATAJIRI AMBAO HAWANA SHIDA YA FTARI KWENYE MAHOTELI YA KITALII
NATOA WITO KWA WENGINE WAENDE MAHOSPTITAL KAMA YA AMANA, TEMEKE, MWANANYAMALA NK HUKO HALI MBAYA WAACHE KUFUTURISHA SERENA HOTEL
aise besti mmefanya kitu cha maana sana.
ReplyDeleteChe
Ukiachia futari mmefanya jambo kubwa sana mmewapa faraja kubwa sana wagonjwa hawa, bila shaka wamejisikia furaha na amani mioyoni mwao.
ReplyDelete