Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi  Serikalini (GEPF), Anselim Peter akitoa pole kwa wagonjwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam wakati wafanyakazi wa mfuko huo waliposhiriki futari na wagonjwa waliolazwa katika taasisi hiyo. Kushoto ni Meneja Masoko wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina
 Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi  Serikalini (GEPF), Anselim Peter akiandaa futari kwa mmoja wa wagonjwa hao.
 Meneja Masoko wa Mfuko huo, Aloyce Ntukamazina akimpa futari mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road.
 Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi  Serikalini (GEPF), Anselim Peter akishirikiana na baadhi ya ndugu wa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road kugawa ftari.
 Baadhi ya wagonjwa wakipata futari.
Mkurugenzi Uendeshaji wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi  Serikalini (GEPF), Anselim Peter pamoja na Menja Masoko wa mfuko huo, Aloyce Ntukamazina kulia wakishiriki futari pamoja na wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Saratani Ocean Road jijini Dar es Salaam.Picha na Francis Dande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hongereni Mfuko wa GEPF kwa kuwafikiria wagonjwa wa Saratani tumeona Mifuko mingine ikifuturisha Kempisky au Movenpick tena kwa wafanyakazi wenye uwezo. Keep it up

    ReplyDelete
  2. Hongereni GEPF kwa kufuturisha wagonjwa wa saratani tumeshuhudia mifuko mingine ikifuturisha Kempisky au Movenpick kwa wafanyakazi wao wenye uwezo. Keep it up

    ReplyDelete
  3. Nawasifu sana GEPF kwa kufuturisha wahitaji halisi, kweli huu ni Mfuko unaoilenga jamii. Hongereni sana, na wengine mfuate sasa !!!!

    ReplyDelete
  4. bila shaka mmeipeleka futari inapotakiwa

    ReplyDelete
  5. Ahsanteni GEPF kwa kuijali na kushirikiana na Jamii katika Mfungo wa Ramadhani.

    ReplyDelete
  6. GEPF mmefanya jambo jema sana kwa kutoa futari kwa wagonjwa ambao inawezekana sio wafanyakazi wa Mfuko au pia huenda wasiwe wateja wa Mfuko, isipokuwa Mfuko wa PPF sikuwaelewa walipojiandalia futari Wafanyakazi wa Mfuko!!!

    ReplyDelete
  7. Hivi kweli unaenda kutoa msaada wa futari halafu chakula unapakulia mfuniko wa plastiki? kweli hii si dharau,mmeshindwa kabisa hata kununua vijiko kwa ajili ya kupakulia chakula? mnakudhalilisha na kukitia aibu chombo cha serikali kwa kweli.

    ReplyDelete

  8. NAWAPONGEZA SANA GEPF KWA KUFUTURISHA WAGONJWA. HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA KUWA SIO KAMA MASHIRKA MENGINE YANAYO FUTIRISHA MATAJIRI AMBAO HAWANA SHIDA YA FTARI KWENYE MAHOTELI YA KITALII

    NATOA WITO KWA WENGINE WAENDE MAHOSPTITAL KAMA YA AMANA, TEMEKE, MWANANYAMALA NK HUKO HALI MBAYA WAACHE KUFUTURISHA SERENA HOTEL

    ReplyDelete
  9. aise besti mmefanya kitu cha maana sana.

    Che

    ReplyDelete
  10. Ukiachia futari mmefanya jambo kubwa sana mmewapa faraja kubwa sana wagonjwa hawa, bila shaka wamejisikia furaha na amani mioyoni mwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...