Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa
ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi
Ras-Fumba Zanzibar,wenye urefu wa 37 Kilomita, katika Bandari ya
Malindi ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini
Japan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akisalimiana na Msaidizi Mtendaji
Mkuu wa MCA-T kwa upande wa Zanzibar, Bw,Ahmed Rashid,alipowasili
katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,kuupokea na kuukagua waya
huo wa Umeme ,utakaolazwa kwa siku Kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni
Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar. [Picha na Ramadha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,( kushoto) akifuatana na Waziri wa Ardhi
Makaazi Maji na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban,alipofika katika
Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,Kuupokea na Kuukagua Waya wa
Baharini utakaotumika katika Mradi wa Ulazaji waya wa pili wa Umeme
kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar,ukiwa katika
Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Rais Dk Ali Mohd Shein kuupokea Waya Mpya wa Umeme wenye uwezo wa kuchukua Megawati 100.kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar.


Hili suala lishakuwa la kisiasa eeh. By the way walitakiwa kuvaa helmet lakini tahadhari ziro!
ReplyDeletehaya wale ndugu zetu wasiotaka muungano umeme huo tunawaletea mkitufanyia ukorofi tunauzima tu mnabaki nchi nzima giza hamuonani
ReplyDeleteHaya wale wanaodai Muungano uvunjike kwa madai kuwa Zenji wanaodhulumiwa wapo wapi? Mnaonaje mkijitokeza muda huu kugombania haki zenu..... Afu nashindwa kuelewa kama Bara umeme wenyewe ni kwa kudonoa donoa mgao kila siku tutawezaje kutosheleza mahitaji ya Zenji kama kiwango tunachozalisha hakitoshi?
ReplyDeleteni jambo la kupokelewa na waziri husika na mkurugenzi wa bandari.
ReplyDeletemi naona raisi is too exaggeration jamani.
Jamani, magari na watu wa usalama watoke Ikulu na barabara zifungwe kwa ajili ya rais kwenda kupokea waya wa umeme!! Me nadhani watu wa protocal mara nyingine wanakuwa wanafanya makosa kwa ziara kama hizi kwa Rais.......waya wa umeme unamhitaji Rais kivipi sasa? Kuna waziri husika na viongozi wengine wengi tu.....
ReplyDelete