Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar,wenye urefu wa 37 Kilomita, katika Bandari ya Malindi ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akisalimiana na Msaidizi Mtendaji Mkuu wa MCA-T kwa upande wa Zanzibar, Bw,Ahmed Rashid,alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,kuupokea na kuukagua waya huo wa Umeme ,utakaolazwa kwa siku Kumi na mbili kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar. [Picha na Ramadha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,( kushoto) akifuatana na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati,Ramadhan Abdalla Shaaban,alipofika katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo,Kuupokea na Kuukagua Waya wa Baharini utakaotumika katika Mradi wa Ulazaji waya wa pili wa Umeme kutoka Ras-Kiromoni Dar es Salaam hadi Ras-Fumba Zanzibar,ukiwa katika Meli ya Kampuni ya Viscas kutoka nchini Japan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Zanzibar Hassan Ali Mbarouk akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Rais Dk Ali Mohd Shein kuupokea Waya Mpya wa Umeme wenye uwezo wa kuchukua Megawati 100.kutoka Tanzania Bara hadi Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Hili suala lishakuwa la kisiasa eeh. By the way walitakiwa kuvaa helmet lakini tahadhari ziro!

    ReplyDelete
  2. haya wale ndugu zetu wasiotaka muungano umeme huo tunawaletea mkitufanyia ukorofi tunauzima tu mnabaki nchi nzima giza hamuonani

    ReplyDelete
  3. Haya wale wanaodai Muungano uvunjike kwa madai kuwa Zenji wanaodhulumiwa wapo wapi? Mnaonaje mkijitokeza muda huu kugombania haki zenu..... Afu nashindwa kuelewa kama Bara umeme wenyewe ni kwa kudonoa donoa mgao kila siku tutawezaje kutosheleza mahitaji ya Zenji kama kiwango tunachozalisha hakitoshi?

    ReplyDelete
  4. ni jambo la kupokelewa na waziri husika na mkurugenzi wa bandari.
    mi naona raisi is too exaggeration jamani.

    ReplyDelete
  5. Jamani, magari na watu wa usalama watoke Ikulu na barabara zifungwe kwa ajili ya rais kwenda kupokea waya wa umeme!! Me nadhani watu wa protocal mara nyingine wanakuwa wanafanya makosa kwa ziara kama hizi kwa Rais.......waya wa umeme unamhitaji Rais kivipi sasa? Kuna waziri husika na viongozi wengine wengi tu.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...