Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Saada Mkuya Salum akizinduwa rasmi Benki ya Amana Kariakoo jijini Dar es salaam leo huku wakurugenzi Dr Idriss Rashid (aliyeshika mwamvuli) na Bw. Haroon Pirmohamed wakishuhudia. Amana Bank
inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na
malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata
Sharia kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwa kutumia
teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja wetu wote.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchimi Mh. Saada Mkuya (Kushoto) akimpongeza Branch Manager Bi Warda huku wakurugenzi Dr Idriss Rashid na Bw. Haroon Pirmohamed
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Saada Mkuya Salum (Kati) akiwa na Wakurungenzi wa Benki ya Amana mara baada ya kuizindua rasmi benki hiyo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Amana Bank wakipozi kwa furaha na fahari baada ya uzinduzi huo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA
Ni benk ya kiislam? mana naona mana naona wadada wote wamevaa ushungi.
ReplyDeleteNyerere alisema" mvisa visa maradhi a kilalo kirambura"
ReplyDeletemaanake ni mficha ficha maradhi kilio kitamuumbua. watu tuna-comment kuhusu udini wewe unakataa kuweka comment zetu.. we michuzi nini wewe! mtoto wako hataishi tanzania uliyoishi kwa sababu hii generation ndo ya mwisho kuishi kwa amani tanzania.... udini mwingi mno hata wewe michuzi mdini mimi mwenyewe mdini, tia akili hapo.
we anony wa kwanza umeangalia picha tu bila kusoma... ungesoma usingeuliza hilo swali
ReplyDeleteIgnorant
maelezo yapo katika picha maneno mengi mengi ya nini hapo akili kumkichwa.
ReplyDeleteAl Habib Michuzi
ReplyDeleteMimi ni mdau na niko New York na nimevutiwa sana na huyu Bi Warda.
Je ana mume? au single?
Kama Single bas mimi niko tayari kufanya mpango wa kuja kutoa posa.
Mdau,
ReplyDeleteWewe anon wa PILI point yako nini?
Benki ya kiislamu SIYO udini, kwa kifupi hili neno UDINI halina maana kabisa, aliyelianzisha ndiye aliyejua kinachoendelea.
Pale mwenge EFATHA kuna benki, hiyo nayo imekaaje.
ReplyDeleteNeno "Islamic banking” ni mfumo wa shughuli za kibenki zinazoendeana na kukubaliana na Sheria za Kiislamu, na zinazoongozwa na Islamic economics.
Hususan, Sheria ya Kiislamu inakataza Riba (Interest),
Kwa nyongeza, Sheria ya Kiislamu inapiga marufuku kuwekeza kwenye biashara haramu kwenye Uislamu kama Pombe au nguruwe au biashara zinazotoa huduma za kihabari kama Magazeti ya udaku au ngono vitu ambavyo ni kinyume na maadili ya kiislamu.
Hakuna 'udini' hapa, maana baadhi yetu tukisikia sharia law tunapata picha ya kukatwa mkono, shingo au kupigwa mawe.
Tufanye utafiti kabla ya kukimbilia "mvisavisa maradhi a kilalo kirambura"
huyo mdau wa pili naye, udini udini,mbona Mkombozi Bank wamejaa wakristo watupu? mbona husemi kama ni udini? bora hata hiyo Amana Bank wanaajiri na wakristo, huko Mkombozi hawataki hata kusikia uislam wala jina la kiislam, nini waislam, hata dhehebu lingine huajiriwi Mkombozi Bank zaidi ya Roman Catholic tu, hilo nalo unalizungumziaje?
ReplyDeleteNaona watu nchi hii wana hamu ya vita maana siku hizi imekua mambo mengi ni UDINI.
ReplyDeleteAmani iliyopo mnaona sio nzuri mnataka vurugu sijui mtakimbilia wapi wakati majirani zetu wote kwao hakuna amani. DRC, Burundi, Kenya na mashambulio ya Al-Shabaab, Uganda, Rwanda.
Ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki wamezika kw aheshima zote za dini zao na wamestirika, tulibaki hatujui tutakufa vipi na wapi..
Good, proud of it, i neeed to invest with them coz it is so easy and straight profit you can make money comapre to other banks...
ReplyDelete