Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Saada Mkuya Salum akizinduwa rasmi Benki ya Amana Kariakoo jijini Dar es salaam leo huku  wakurugenzi Dr Idriss Rashid (aliyeshika mwamvuli) na Bw. Haroon Pirmohamed wakishuhudia. Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata Sharia kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja wetu wote.
 
 Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchimi Mh. Saada Mkuya (Kushoto) akimpongeza Branch Manager Bi Warda huku wakurugenzi Dr Idriss Rashid na Bw. Haroon Pirmohamed

 Naibu  Waziri wa  Fedha na Uchumi Mh. Saada Mkuya Salum (Kati) akiwa na Wakurungenzi wa Benki ya Amana mara baada ya kuizindua rasmi benki hiyo
Baadhi ya Wafanyakazi wa Amana Bank wakipozi kwa furaha na fahari baada ya uzinduzi huo. Kwa habari kamili BOFYA HAPA



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Ni benk ya kiislam? mana naona mana naona wadada wote wamevaa ushungi.

    ReplyDelete
  2. Nyerere alisema" mvisa visa maradhi a kilalo kirambura"
    maanake ni mficha ficha maradhi kilio kitamuumbua. watu tuna-comment kuhusu udini wewe unakataa kuweka comment zetu.. we michuzi nini wewe! mtoto wako hataishi tanzania uliyoishi kwa sababu hii generation ndo ya mwisho kuishi kwa amani tanzania.... udini mwingi mno hata wewe michuzi mdini mimi mwenyewe mdini, tia akili hapo.

    ReplyDelete
  3. we anony wa kwanza umeangalia picha tu bila kusoma... ungesoma usingeuliza hilo swali

    Ignorant

    ReplyDelete
  4. maelezo yapo katika picha maneno mengi mengi ya nini hapo akili kumkichwa.

    ReplyDelete
  5. Al Habib Michuzi

    Mimi ni mdau na niko New York na nimevutiwa sana na huyu Bi Warda.

    Je ana mume? au single?

    Kama Single bas mimi niko tayari kufanya mpango wa kuja kutoa posa.

    Mdau,

    ReplyDelete

  6. Wewe anon wa PILI point yako nini?

    Benki ya kiislamu SIYO udini, kwa kifupi hili neno UDINI halina maana kabisa, aliyelianzisha ndiye aliyejua kinachoendelea.

    Pale mwenge EFATHA kuna benki, hiyo nayo imekaaje.

    ReplyDelete

  7. Neno "Islamic banking” ni mfumo wa shughuli za kibenki zinazoendeana na kukubaliana na Sheria za Kiislamu, na zinazoongozwa na Islamic economics.

    Hususan, Sheria ya Kiislamu inakataza Riba (Interest),
    Kwa nyongeza, Sheria ya Kiislamu inapiga marufuku kuwekeza kwenye biashara haramu kwenye Uislamu kama Pombe au nguruwe au biashara zinazotoa huduma za kihabari kama Magazeti ya udaku au ngono vitu ambavyo ni kinyume na maadili ya kiislamu.

    Hakuna 'udini' hapa, maana baadhi yetu tukisikia sharia law tunapata picha ya kukatwa mkono, shingo au kupigwa mawe.

    Tufanye utafiti kabla ya kukimbilia "mvisavisa maradhi a kilalo kirambura"

    ReplyDelete
  8. huyo mdau wa pili naye, udini udini,mbona Mkombozi Bank wamejaa wakristo watupu? mbona husemi kama ni udini? bora hata hiyo Amana Bank wanaajiri na wakristo, huko Mkombozi hawataki hata kusikia uislam wala jina la kiislam, nini waislam, hata dhehebu lingine huajiriwi Mkombozi Bank zaidi ya Roman Catholic tu, hilo nalo unalizungumziaje?

    ReplyDelete
  9. Naona watu nchi hii wana hamu ya vita maana siku hizi imekua mambo mengi ni UDINI.
    Amani iliyopo mnaona sio nzuri mnataka vurugu sijui mtakimbilia wapi wakati majirani zetu wote kwao hakuna amani. DRC, Burundi, Kenya na mashambulio ya Al-Shabaab, Uganda, Rwanda.

    Ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki wamezika kw aheshima zote za dini zao na wamestirika, tulibaki hatujui tutakufa vipi na wapi..

    ReplyDelete
  10. Good, proud of it, i neeed to invest with them coz it is so easy and straight profit you can make money comapre to other banks...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...