Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa  na askari wa jeshi la Polisi  baada ya vita ya kurushiana risasi baada ya jaribio la kupora kusambaratishwa na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia 
 Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa  kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. mchezo mchafu tunaujuwa longtime kama majambazi wa tanzania ni wanajeshi na polisi wenyewe tokea miaka hiyo

    ninasema hayo nina ushahidi nayo maana mwaka 1998 tulikuwa tunasafiri na fuso kuelekea dodoma pale maeneo ya msamvu morogoro tukasimamishwa na polisi wa barabarani

    baada ya kusimama walitokea wenzao kwenye kichaka na kutufunga kamba mikononi na kutupeleka polini wakachukua gari la mizigo na kuenda kushusha mzigo wote

    baadae wakaliacha fuso letu sehemu nyingine mali zote wameiba

    na baada ya wiki moja kupita polisi wa kituo cha msimbazi wakaiba hela za mishahara yao zilizokuwa zimehifadhiwa kwa mkuu wa kituo

    hayo yametokea mengi sana kutokana na njaa za polisi wetu na wanajeshi wanaoitwa majina ya walinzi wa raia

    hali ni mbaya sana kimapato kiasi kwamba tunapoelekea kuna hatari majambazi wanajeshi wakasahambulia matajiri badili ya kupambana na vita za maadui wetu.

    tunaomba wahusika wakuu wa jeshi na polisi wawajibishwe kwani hali sio njema tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...