Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha bunduki zilizokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi ambapo watatu kati yao walijeruhiwa na askari wa jeshi la Polisi baada ya vita ya kurushiana risasi baada ya jaribio la kupora kusambaratishwa na kisha kufariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha kitako cha bunduki aina ya Rifle iliyokutwa kwenye begi la watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi. Watatu kati yao walijeruhiwa kwa risasi na askari wa jeshi la polisi na kisha kufariki dunia
Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akionyesha sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ0 ambazo zilikutwa kwenye begi la watu watano ambao wanasadikiwa kuwa ni majambazi .Tukio hilo lililtokea katika eneo la Olmatejoo jijini Arusha leo asubuhi na Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi Watatu kati yao ambao baadae walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali.Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha


mchezo mchafu tunaujuwa longtime kama majambazi wa tanzania ni wanajeshi na polisi wenyewe tokea miaka hiyo
ReplyDeleteninasema hayo nina ushahidi nayo maana mwaka 1998 tulikuwa tunasafiri na fuso kuelekea dodoma pale maeneo ya msamvu morogoro tukasimamishwa na polisi wa barabarani
baada ya kusimama walitokea wenzao kwenye kichaka na kutufunga kamba mikononi na kutupeleka polini wakachukua gari la mizigo na kuenda kushusha mzigo wote
baadae wakaliacha fuso letu sehemu nyingine mali zote wameiba
na baada ya wiki moja kupita polisi wa kituo cha msimbazi wakaiba hela za mishahara yao zilizokuwa zimehifadhiwa kwa mkuu wa kituo
hayo yametokea mengi sana kutokana na njaa za polisi wetu na wanajeshi wanaoitwa majina ya walinzi wa raia
hali ni mbaya sana kimapato kiasi kwamba tunapoelekea kuna hatari majambazi wanajeshi wakasahambulia matajiri badili ya kupambana na vita za maadui wetu.
tunaomba wahusika wakuu wa jeshi na polisi wawajibishwe kwani hali sio njema tanzania.