Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda akisisitiza jambo kwa katika Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika  Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika   jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa  Kikao hicho
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa  Kikao
 
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Kikao Kazi cha tisa cha  Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini  (hawapo Pichani).Kikao hicho kilifanyika Jijini Dar es Salaam  na kauli mbiu ilikuwa ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe Chachu ya Maendeleo. 

Wadau wa Sekta ya Utamaduni  nchini wakimsikiliza Wazari wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara  (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi  wa Kikao kazi cha tisa cha sekta hiyo kilichofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo. Picha zote  na Benjamin Sawe wa WHVUM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. huyu mama mimi ananifurahisha na hii twende kilioni yake sio wengine na joto hili wanaenda kuongeza mawigi na maweaving!!

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa we mdau wa kwanza,Mukangara ananifurahisha kwa kuendelea kudumisha mitindo asilia ya nywele, twende kilioni murua kabisa, keep it up.

    ReplyDelete
  3. Huyu ni mfano mzuri sana kwa sisi watu weusi na ugonjwa wetu wa kutojiamini na kuiga watu weupe.Hivi mnamuona anavyopendeza?hongera sana waziri wafundishe.

    ReplyDelete
  4. NI KWELI KABISA HUYU WAZIRI ANASTAHILI PONGEZI KAMA WALIVYOSEMA WALIOTANGULIA, SIKU HIZI UKIKUTANA NA WANAWAKE HAPA TANZANIA IWE NJIANI AU KTK SHEREHE NA POPOTE PALE HUJUI NI WA NCHI GANI KWA MAANA HAYO MACHUBUZI NA HIYO MINYWELE YA BANDIA WOTE WAMEKUWA MACHOTARA. MKATAA KWAO MTUMWA. NA WANAUME WENGINE WAVIVU KUCHANA BASI MAPARA KILA SIKU, ZAMANI UKINYOA KIPARA LAZIMA UPEWE POLE KWA MAANA NI ISHARA KUWA UMEFIWA. TUPENDE TULIVYOZALIWA ILA TUWE WASAFI/WATANASHATI/
    MARIDADI/WAREMBO KWA ASILI TULIYO NAYO SIO KUJIBADILISHABADILISHA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...