Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda
akisisitiza jambo kwa katika Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni
kilichofanyika Jijini Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Kikao hicho ni
Urasimishaji wa tasnia za Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo.Kushoto ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi
Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni
kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiteta jambo na Katibu Mkuu Bw. Sethi
Kamuhanda wakati wa Kikao cha tisa cha wadau wa Sekta ya Utamaduni
kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza
Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa Kikao hicho
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akimpongeza
Mghani Mashairi Bwana Mohamed Lukemo wakati wa ufunguzi wa Kikao
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Kikao
Kazi cha tisa cha Wadau wa Sekta ya Utamaduni
nchini (hawapo Pichani).Kikao hicho
kilifanyika Jijini Dar es Salaam na kauli mbiu ilikuwa ni Urasimishaji
wa tasnia za Filamu na Muziki uwe Chachu ya Maendeleo.
Wadau wa Sekta ya Utamaduni nchini wakimsikiliza Wazari wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara
(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi
wa Kikao kazi cha tisa cha sekta hiyo kilichofanyika Jijini Dar es
Salaam hivi karibuni.Kauli mbiu ya Kikao hicho ni Urasimishaji wa tasnia za
Filamu na Muziki uwe chachu ya Maendeleo. Picha zote na Benjamin Sawe wa WHVUM.


huyu mama mimi ananifurahisha na hii twende kilioni yake sio wengine na joto hili wanaenda kuongeza mawigi na maweaving!!
ReplyDeleteNi kweli kabisa we mdau wa kwanza,Mukangara ananifurahisha kwa kuendelea kudumisha mitindo asilia ya nywele, twende kilioni murua kabisa, keep it up.
ReplyDeleteHuyu ni mfano mzuri sana kwa sisi watu weusi na ugonjwa wetu wa kutojiamini na kuiga watu weupe.Hivi mnamuona anavyopendeza?hongera sana waziri wafundishe.
ReplyDeleteNI KWELI KABISA HUYU WAZIRI ANASTAHILI PONGEZI KAMA WALIVYOSEMA WALIOTANGULIA, SIKU HIZI UKIKUTANA NA WANAWAKE HAPA TANZANIA IWE NJIANI AU KTK SHEREHE NA POPOTE PALE HUJUI NI WA NCHI GANI KWA MAANA HAYO MACHUBUZI NA HIYO MINYWELE YA BANDIA WOTE WAMEKUWA MACHOTARA. MKATAA KWAO MTUMWA. NA WANAUME WENGINE WAVIVU KUCHANA BASI MAPARA KILA SIKU, ZAMANI UKINYOA KIPARA LAZIMA UPEWE POLE KWA MAANA NI ISHARA KUWA UMEFIWA. TUPENDE TULIVYOZALIWA ILA TUWE WASAFI/WATANASHATI/
ReplyDeleteMARIDADI/WAREMBO KWA ASILI TULIYO NAYO SIO KUJIBADILISHABADILISHA.