Mwenyekiti wa Muungano wa vikundi vya kuweka na kukopa (UVIMA), Tatu Mgao (kulia), akitoa shukurani kwa WAMA na NHIF kuwawezesha wanachama wa umoja huo kujiunga na masuala ya matibabu ya mfuko huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Athuman Rehani, Mkurugenzi wa Operesheni wa NHIF, Eugen Mikongoti na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wanawake wa WAMA, Tabu Likoko.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananwake wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Tabu Likoko akiwahamasisha wanawake wa Umoja wa Vikundi vya kuweka na Kukopa (UVIMA), wakati wa hafla ya wanachama wa wa umoja huo kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Majohe, Ilala, Dar es Salaam leo.
Wanachama wa Uvima wakishangilia baada ya kutangaziwa na uongozi wa NHIF , wamekubaliwa kujiunga na mfuko huo ambapo watakaonufaika kwa kulipia ada ya sh. 10,600 kwa mwezi ni watu sita, ambao ni mama, baba na watoto wao wanne.
| Baadhi ya wanachama wa Uvima wakiandikishwa kujiunga na mfuko huo. |


Hakuna serikali inayo sadia wakinamama mambo sasa ya dini tu. Ukitaka kufanikiwa jiunge na chama cha dini kwenye kanisa, mskitini, temple au organization zinazo endlea kutimia dini kusaidia wakinamama.Kushindwa kudanganya ni viyama winavyo endlea kutimiwa na mifisadi.
ReplyDelete