Familia ya Marehemu Alhaj Mbarouk Kassim Mwandoro wa Dares Salaam wanapenda kutoa shukurani zadhatikwa Ndugu, Jamaa,Majirani, Marafiki na watu wote kwa Ujumla kwa msaada wenu mkubwa  wakati wakipindi kigumu cha msiba kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa Alhaj MbaroukKassim Mwandoro  aliyefariki dunia tarehe 13/11/2012 katika hospitali ya Hindu Mandal nakuzikwa tarehe 14/11/2012 katika makaburi ya Kisutu, Dar es salaam.

Pia tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu nasi kwa dua na maombi wakati wote hadi tulipompumzisha  baba yetu Mpenzi
Tunatoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya. M. Kikwete.

Tunawakaribisha wote kwenye Arobaini ya marehemu, Mkesha utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 21/12/2012 nakufuatiwa na Khitma itakayosomwa Jumamosit arehe 22/12/2012 kuanzia saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu 351 Ali Bin Said Rd , Oyster Bay ,Dar es Salaam.


Inna lillah wa Inna lillayhi Rajiun.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ?NOVEMBA 22, JUMAMOSSI 2012. ankal angalia vizuri naona umekosea kichwa cha habari.

    ReplyDelete

  2. Mwenyezi Mungu amlaze Mhe. Mwandoro pema peponi, Amen.

    ReplyDelete
  3. Innah lillahi wainnah illahi rajiun - wewe umetangulia na sisi tuko nyuma yako baba. Mwenyezi mungu akulaze pema peponi,akupunguzie adhabu za kaburi baba, akupe daraja baba. Amin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...