Familia ya
Marehemu Alhaj Mbarouk Kassim Mwandoro wa Dares Salaam wanapenda kutoa shukurani
zadhatikwa Ndugu, Jamaa,Majirani, Marafiki na watu wote kwa Ujumla kwa msaada wenu
mkubwa wakati wakipindi kigumu cha msiba
kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha shughuli za msiba wa baba yetu mpendwa
Alhaj MbaroukKassim Mwandoro aliyefariki
dunia tarehe 13/11/2012 katika hospitali ya Hindu Mandal nakuzikwa tarehe
14/11/2012 katika makaburi ya Kisutu, Dar es salaam.
Pia tunawashukuru kwa jinsi mlivyokuwa karibu nasi kwa dua na maombi wakati
wote hadi tulipompumzisha baba yetu
Mpenzi
Tunatoa
shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya. M. Kikwete.
Tunawakaribisha
wote kwenye Arobaini ya marehemu, Mkesha utafanyika siku ya Ijumaa tarehe
21/12/2012 nakufuatiwa na Khitma itakayosomwa Jumamosit arehe 22/12/2012 kuanzia
saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu 351 Ali Bin Said Rd , Oyster Bay ,Dar es
Salaam.
Inna
lillah wa Inna lillayhi Rajiun.
?NOVEMBA 22, JUMAMOSSI 2012. ankal angalia vizuri naona umekosea kichwa cha habari.
ReplyDelete
ReplyDeleteMwenyezi Mungu amlaze Mhe. Mwandoro pema peponi, Amen.
Innah lillahi wainnah illahi rajiun - wewe umetangulia na sisi tuko nyuma yako baba. Mwenyezi mungu akulaze pema peponi,akupunguzie adhabu za kaburi baba, akupe daraja baba. Amin
ReplyDelete