Tanzania ni miongoni mwa nchi tano zilizochaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Marekani la Changamoto za Milenia, yaani Millenium Challenge Corporation (MCC) kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha kwa awamu nyingine tena.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya MCC katika kikao chake kilichofanyika tarehe 19 Desemba, 2012 imebainisha majina ya nchi tano zenye sifa ya kupatiwa msaada huo wa fedha kutoka MCC kuwa ni Tanzania, Liberia, Niger, Sierra Leone na Morocco. 
Hivi sasa nchi hizo zinatakiwa kuandaa mapendekezo ya mipango yao ya maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha kwa awamu nyingine. 
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji wa MCC, Bwana Daniel W. Yohannes, Tanzania na Morocco zimeendelea kufanya vizuri katika matumizi ya fedha za MCC zilizotolewa katika Awamu ya Kwanza na akabainisha kuwa nchi hizo zimekuwa washirika wazuri katika suala zima la utekelezaji.  Sifa za kupatiwa fedha kutoka MCC kwa awamu nyingine zinategemea utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo inayojielekeza zaidi katika shughuli za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
 Katika Awamu ya Kwanza, Tanzania ilipatiwa msaada wa fedha kutoka MCC wa jumla ya Dola za Marekani 698.1 milioni ambazo zimetumika katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kupunguza umaskini hapa nchini.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
20 Desemba, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Naomba kushauri. Haitoshi kusema fedha za MCC zimetumika kutekeleza mipango mbali mbali kwa lengo la kupunguza umaskini! Tueleze ni mipango ama miradi ipi. Mbona Serikali hii imefanya mengi! Kwanini tusitaje hizo barabara, shule, vituo vya afya ama viwanda vilivyofaidika na msaada huo ili tuuone wa msaada huo na maisha ama maendeleo yetu? Lazima kila fursa tujipigie wenyewe debe!. Zitto Kabwe hawezi kufanya hilo!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hii inawezekana Tz tu 'Kushaingilia Kusaidiwa' mimi nilidhani wakati ufike tushangilie kuwa na bajeti isiyotegemea misaada zaidi ya hapo ni masikitiko tupu

    ReplyDelete
  3. Hiyo mipango mbalimbali ya maendeleo haina haina majina?

    ReplyDelete
  4. Mimi sina ugomvi kabisa na taarifa ya hayo yaliyofanyika . yote ni mema. Tatizo nililo nalo mimi ni jinsi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Raisi inavyowasilisha taarifa zake mara kwa mara. Kutumia karatasi rasmi ya kiofisi yenye nembo iliyoandikwa kwa kiingereza kisha taarifa ikatolewa kwa Kiswahili , Mimi nadhani haijatulia sana. Nashauri kurugenzi iaandae karatasi hii maalum yenye nembo kwa lugha ya kiswahili kwa ajili ya taarifa za kiswahili . Hii ya sasa waitumie kwa taarifa za kiingereaa , au njia mbadala ni kuandaa karatasi hii muhimu ikiwa nalugha zote mbili ili ikidhi matumizi kwa lugha zote mbili kwa kadri ya matakwa ya kurugenzi kutegemea ni walengwa wapi waliokusudiwa kupewa taarifa hiyo.
    mfano mzuri ni karatasi yenye nembo wanayotumia Benki Kuu ya Tanzania . Naomba kutoa hoja.
    MAKMKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...