Tanzania
ni miongoni mwa nchi tano zilizochaguliwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Marekani
la Changamoto za Milenia, yaani Millenium
Challenge Corporation (MCC) kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha kwa awamu
nyingine tena.
Taarifa
iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya MCC
katika kikao chake kilichofanyika tarehe 19 Desemba, 2012 imebainisha majina ya
nchi tano zenye sifa ya kupatiwa msaada huo wa fedha kutoka MCC kuwa ni
Tanzania, Liberia, Niger, Sierra Leone na Morocco.
Hivi
sasa nchi hizo zinatakiwa kuandaa mapendekezo ya mipango yao ya maendeleo kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali, kwa ajili ya kupatiwa msaada wa fedha kwa
awamu nyingine.
Kwa
mujibu wa Afisa Mtendaji wa MCC,
Bwana Daniel W. Yohannes, Tanzania na Morocco zimeendelea kufanya vizuri katika
matumizi ya fedha za MCC zilizotolewa
katika Awamu ya Kwanza na akabainisha kuwa nchi hizo zimekuwa washirika wazuri katika
suala zima la utekelezaji. Sifa za
kupatiwa fedha kutoka MCC kwa awamu
nyingine zinategemea utekelezaji mzuri wa mipango ya maendeleo inayojielekeza zaidi
katika shughuli za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Katika
Awamu ya Kwanza, Tanzania ilipatiwa msaada wa fedha kutoka MCC wa jumla ya Dola za Marekani 698.1 milioni ambazo zimetumika
katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kupunguza
umaskini hapa nchini.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
20 Desemba,
2012
Naomba kushauri. Haitoshi kusema fedha za MCC zimetumika kutekeleza mipango mbali mbali kwa lengo la kupunguza umaskini! Tueleze ni mipango ama miradi ipi. Mbona Serikali hii imefanya mengi! Kwanini tusitaje hizo barabara, shule, vituo vya afya ama viwanda vilivyofaidika na msaada huo ili tuuone wa msaada huo na maisha ama maendeleo yetu? Lazima kila fursa tujipigie wenyewe debe!. Zitto Kabwe hawezi kufanya hilo!!!!!
ReplyDeleteHii inawezekana Tz tu 'Kushaingilia Kusaidiwa' mimi nilidhani wakati ufike tushangilie kuwa na bajeti isiyotegemea misaada zaidi ya hapo ni masikitiko tupu
ReplyDeleteHiyo mipango mbalimbali ya maendeleo haina haina majina?
ReplyDeleteMimi sina ugomvi kabisa na taarifa ya hayo yaliyofanyika . yote ni mema. Tatizo nililo nalo mimi ni jinsi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Raisi inavyowasilisha taarifa zake mara kwa mara. Kutumia karatasi rasmi ya kiofisi yenye nembo iliyoandikwa kwa kiingereza kisha taarifa ikatolewa kwa Kiswahili , Mimi nadhani haijatulia sana. Nashauri kurugenzi iaandae karatasi hii maalum yenye nembo kwa lugha ya kiswahili kwa ajili ya taarifa za kiswahili . Hii ya sasa waitumie kwa taarifa za kiingereaa , au njia mbadala ni kuandaa karatasi hii muhimu ikiwa nalugha zote mbili ili ikidhi matumizi kwa lugha zote mbili kwa kadri ya matakwa ya kurugenzi kutegemea ni walengwa wapi waliokusudiwa kupewa taarifa hiyo.
ReplyDeletemfano mzuri ni karatasi yenye nembo wanayotumia Benki Kuu ya Tanzania . Naomba kutoa hoja.
MAKMKA