Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth Natongo Zziwa akifungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa wabunge wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya ambayo hafanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda, Bunrundi, Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote ambao wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.
Kikosi cha Uganda: Baada ya uzinduzi timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la Afrika Mashariki ndizo zilizofungua dimba ambapo zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Mechi itakayofuata ni kati ya Tanzania na Kenya.







africa khususan ya mashariki kamwe haitoweza kupiga vita umaskini na kupata maendeleo,hii michezo ni kupeana posho tu hakuna faida yoyote inayopatikana kutokana na michezo hii.hizi pesa wangeziwekeza kwenye michezo mashuleni ili watoto waendeleze vipaji,hawa watu wazima wameshazeeka,kwanini wapewe posho kwa afya zao wenyewe,kwa kweli inasikitisha,michezo ya namna hii ipo africa tu
ReplyDeleteGreat point above, nchi inaliwa utafikiri hakuna kesho. Hizo ni hela zetu, hao wenye matumbo wangetumia hela zao kwenda kutalii Nairobi. Guys show some leadership!!! Kuna siku uwajibikaji utaanza, kila kitu kina mwisho.
ReplyDeleteTimu ya Bunge ni Moto Mkali!
ReplyDeleteNi kwa nini kule Kampala-Uganda kwenye CECAFA hamkupeleka timu ta yetu ya Bunge badala yake mnapeleka vijana wasio na 'SHIBE' wa Kili Stars/Taifa Stars?
Mnaona sasa matokeo yake tumeshindwa?