Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Margreth Natongo Zziwa akifungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu na mikono kwa wabunge wa mabunge ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mashindano haya ambayo hafanyika kila mwaka huyakutanisha mabunge ya Tanzania, Kenya, Uganda, Bunrundi, Rwanda pamoja na Bunge la Afrika Mashariki. Kwa mwaka huu Bururndi haikushiri. Mwaka huu mashindono yanafanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi, Kenya. Spika Natongo Zziwa amewashukuru Maspika wote ambao wameziwezesha nchi zao kushiriki mashindano haya.
Maandamano ya uzinduzi
Kikosi cha Tanzania wakati wa uzinduzi.
Kikosi cha Uganda: Baada ya uzinduzi timu ya Bunge la Uganda na timu ya Bunge la Afrika Mashariki ndizo zilizofungua dimba ambapo zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Mechi itakayofuata ni kati ya Tanzania na Kenya.
Kikosi cha Afrika Mashariki
Kikosi cha Tanzania kikiusoma mchezo kati ya Uganda na Afrika Mashariki

Muamuzi wa mchezo huo Bi Damaris Kimani kutoka Kenya.Picha na Prosper Minja-Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. africa khususan ya mashariki kamwe haitoweza kupiga vita umaskini na kupata maendeleo,hii michezo ni kupeana posho tu hakuna faida yoyote inayopatikana kutokana na michezo hii.hizi pesa wangeziwekeza kwenye michezo mashuleni ili watoto waendeleze vipaji,hawa watu wazima wameshazeeka,kwanini wapewe posho kwa afya zao wenyewe,kwa kweli inasikitisha,michezo ya namna hii ipo africa tu

    ReplyDelete
  2. Great point above, nchi inaliwa utafikiri hakuna kesho. Hizo ni hela zetu, hao wenye matumbo wangetumia hela zao kwenda kutalii Nairobi. Guys show some leadership!!! Kuna siku uwajibikaji utaanza, kila kitu kina mwisho.

    ReplyDelete
  3. Timu ya Bunge ni Moto Mkali!

    Ni kwa nini kule Kampala-Uganda kwenye CECAFA hamkupeleka timu ta yetu ya Bunge badala yake mnapeleka vijana wasio na 'SHIBE' wa Kili Stars/Taifa Stars?

    Mnaona sasa matokeo yake tumeshindwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...