Na Happy Katabazi.
Mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la RAJABU ZUBERI (30), mkazi wa Kerege, Muheza, Tanga, akiwa chini ya ulinzi wa Wanausalama leo saa mbili asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, baada kifaa cha upekuzi kumnasa mganga huyo akiwa na vifaa vyake vya uganga ambavyo alikuwa amekuja navyo mahakamani hapo kwa ajili ya kufanyia mambo ya kishirikina katika kesi moja inayomkabili mmoja wa washtakiwa mahakamani hapo.
Hana hata haya aibu imemjaa asijue la kufanya anaomba ardhi ufunguke azame au uje upepo mkali wenye vumbi atimke,mtoto mdogo bado brazamen wa nguvu unashika na kushiriki mambo ya ajabu namna hiyo, wewe ulisikia wapi mambo haya yanafanikisha ktk vitu vyenye asili ya sayansi.
ReplyDeletevifaa vya upekuzi bongo kiboko,mtu anaingia na bastora kwenye ndege havioni lakini Ndumba vinanasa.
ReplyDeleteKwani kukamatwa na vitu vya asili au uganga ni kosa kisheria au wana usalama wana mnyanyasa huyu bwana na kama ni kosa je serikali na viungo vyake vinaamini uchawi???!!!
ReplyDeleteAkijitetea anadumisha mila zake ni kosa la practise his freedom na kuishi huru na kuamini chochote??? kama sheria zinavyosema??
Wanasheria tujadili ili swala.
Jamani AIBU sana tu! Unaesema vitu vya asili sio tatizo ni kweli LAKINI ninavyoelewa vitu vya asili huwa havifichwifichwi sasa huyu jamaa angevaa kiasili kabsa tuelewe moja kwamba anadumisha mila.Huu ni uganga wa kienyeji kabsa jamani kijana anaonekana katoka PASINAA kumbee uchawi mtupu lol aibu...!
ReplyDeleteMi sielewi,,na sielewi kabisa,,,kwanini mtu huyu adhalilishwe namna hii kwa beliefs zake,,,basi na tuambiwe sasa kama SIRIKALI hii inaamini uchawi,,,hawa askari ingetakiwa wamuweke chini ya ulinzi kama angekua na BOMU au VITU VIZITO mtu huyu na sio matunguli haya na mazagazaga yake,,hii ni KUJIDHALILISHA,,,,na ndo maana hata CNN wametuweka kwenye ranks za juu katika mataifa yanayoamini kupita kiasi katika ushirikina.
ReplyDeleteSasa huo uchawi wako mbona haikukusaidia ili usikamatwe?
ReplyDeleteHoja ya msingi hapa ni kuangalia iwapo kati ya "hizo zana za jadi" alizokutwa nazo,kuna chochote ambacho kingeweza kuhatarisha usalama na uhai wa watu waliohudhuria ndani ya mahakama?hapa,vitu ninavyo vizungumzia ni kama kitu chochote chenye ncha kali kama kisu,wembe,mshale,panga,mkuki,;silaha kama bastora,bunduki,grenade,bomu,baruti,kisu cha kivita,nk;au maji yenye sumu,acid,harufu mbaya inayodhuru fahamu,nk;na vinginevyo ambavyo ni hatari kwa binadamu.LAKINI,kama vitu alivyokutwa navyo ni haya Mabuyu yetu ya kienyeji,Tunguli,Hirizi,Ngozi ya ng'ombe au kondoo,Jivu,Shanga,Usinga,Pembe za Tunguli,nk.,"huo ni upuuzi mtupu wa kijadi" ambao hautomfanya mhusika kuonekana na "kosa la kutaka kumdhuru mtu!".tafadhali sana,haya ni maoni yangu binafsi!Maana mhusika,anaweza kudai kwamba,yeye Dini yake au Imani yake ya Kidini ni "Imani za Kijadi",na kwamba,aliamini kwa kuwa na zana zile,angeweza "Kuiomba Miungu Wake",wamsamehe "mtuhumiwa mahakamani aliyemkusudia KUMSAIDIA ILI ASAMEHEWE NA MAHAKAMA",kwa imani na nia njema kabisa za kumsaidia mtuhumiwa "kama vile Wakili au Advocate atakavyo fanya akikusudia kumsaidia mtuhumiwa aepuke hukumu ya mahakama"(the same analogy)! simple analysis! hapo je,wadau? mwachieni huyo jamaa aende zake,bali,atahitaji elimu kidogo!
ReplyDeleteSerikali haina dini na haiamini uchawi mwachilieni dogo mara moja na sayansi yake asilia...ebo!!!!!!
ReplyDeleteKITAMBI NOMA-ARUSHA
aachiwe MGANGA auwawe RAMA JANGILI
ReplyDeleteKAMA SERIKALI YETU INAAMINI HAYA MAMBO BASI NA HII SERIKALI ITAKUWA HAZIMO
ReplyDeleteHUYU MTU NIWAKUACHIWA HURU NA SIO KUMUWEKA CHINI YA ULINZI WA ASKARI HIVI HII INAMAANISHA KWENYE MZUNGUKO WOTE WA SERIKALI INAAMINI HAYA MAMBO NA WANAYAFANYA NA WAO NDIO MAANA WAKAYAOGOPA HAYA MASUALA
SERIKALI IJIANGALIE NA WANACHOKIFANYA, ISIWE SERIKALI YA ABUNUWASI
Duhhh ama kweli mambo ni magumu siku hizi!
ReplyDeleteYaani hata mbinu za Ufundi zinakwama?
TUKIO HILI LITAWAKOSESHA SANA MAPATO YA WEEK END 'MABABU' WANAOTEMBELEWA NA WATEJA WAO KILA MWISHO WA WIKI BAADA YA WATEJA KUDHIHIRISHA KWA KUONA YA KUWA MAMBO YANAKWAMA!
Yaani hawa askari hawana cha kufanya? Tatizo ni kwamba watu wengi wanaamini mauchawi, wasingaamini haya mambo wangecheka na kumfukuzilia mbali huyu mtu aondoke mahakamani. Haya madunguli hayawezi kubadilisha kesi ya huyo mshatikiwa kamwe. Inabidi nchi yetu iamke uchawi haupo tusipoteze muda na pesa kwa imani potovu!
ReplyDeleteJamani elimu ni muhimu sana!
ReplyDeleteUWEZO WA MWENYEZI UPO JUU MNO KULIKO NGUVU ZA UCHAWI !
ReplyDeleteBwana Mdogo Dakta Rajas na mamia kwa maelfu ya Babu zako Madakitari wenzio mmethibitisha hilo kwa matokeo ya zoezi lako kushindwa vilivyo hii leo asubuhi!
MGOSI UMEUMBUKA NA UMETUANGUSHA SANA KTK UMRI HUO KUSHIRIKI VITU HIVYO, PIA TUNASHUKURU SANA LIMEKUWA NI FUNDISHO KWA WENGINE!
LEO HII SAA 2:00 ASUBUHI MCHANA KWEUPE (wala sio usiku wa giza) HAPO MAHAKAMANI KISUTU WEWE MWENYEWE UMETHIBITISHA MGOSI RAJABU ukishuhudia BUNDI akikufia mikononi na usijue la kufanya!
Zoezi limekwama, BUNDI uliyetaka kumrusha kimya kimya hapo Mahakamani ndio kwanza kakufia mikononi!
KWA USANII WENU NA UTAALAMU WENU WA KUBAHATISHA NA KUSIKILIZIA MATOKEO ENDAPO:
1.ZOEZI LINGEFANIKIWA:
Mganga ungejisifu kuwa wewe ni bingwa.
2.ZOEZI LINGEKWAMA:
Mganga ungemlaumu Mteja ya kuwa amekosea Mashariti ama amekiuka Mashariti, SASA IMETOKEA WEWE MWENYEWE BUNDI AMEKUFIA MIKONONI (SIO MTEJA WAKO), SASA JE UTADAI NINI?, KAMA WEWE NDIO DAKITARI UNAWEZA KWELI KUKOSEA MASHARITI?
NI UAMUZI WA BUSARA SERIKALI HASA YA TZ KUZINGATIA KUWA HAINA IBARA ZA SAYANSI KAMA HIZI.
ReplyDeleteNI VILE MARA ZOTE NI ZA KUBAHATISHA NA PATA POTEA!
KAMA DOGO RAJA ALIVYOKWAMA LEO ASUBUHI MAHAKAMANI KISUTU.
Kwa kuwa Mahakama ni ya watu ina Sauti na sauti ya watu ni sauti ya Mwenyezi Mungu!
ReplyDeleteKwa matokeo ya kushindikana kwa zoezi lako la kumchinja paka (ukifikiri huonekani) ukiwasaidia Wateja wako (Wahalifu) ILI KUIPINDISHA SHERIA NA MAAMUZI YA MAHAKAMA ni wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu AMEKATAA KATA KATA!
Hapo ndio tunashuhudia mambo mawili (2):
ReplyDelete1.Dakitari akifariki yeye mwenyewe mbele ya mgonjwa wake aliyekuwa mahututi hajitambui akibaki hai!
2.Punda akifa na mzigo mgongoni!
MGOSI RAJABU ZUBERI,
ReplyDeleteHUWEZI KUWA NA UJASIRI WA KUISHI MAISHA YA WAZI NCHINI KWA AIBU HII ILIYOKUKUTA,
ITABIDI UHAMIE NCHI ZINGINE UKAISHI,
NAKUSHAURI HIVI:
CHUKUA PICHA HII PAMOJA NA RB YA POLISI KWA KISA HIKI UENDE UBALOZI WA MAREKANI UKAOMBE VIZA YA KUPEWA HIFADHI ILI UKAISHI HUKO, KWA KUEPUKA JAMII NA USHAMBULIZI KWA TUHUMA ZA UCHAWI!!!
KIZA KIMETANDA, MATUMAINI MAKUBWA TULIYOYAWEKA KWA WAGANGA YAMEPOTEA!
ReplyDeleteTunashauriwa tuachane na Ushirikina, tuanze mwaka mpya 2013 kwa staili mpya.
Hii ni SALAMU YA KRISMASI na MWAKA MPYA!
Hili ni janga la Taifa!
ReplyDeleteKatika umri mdogo wa miaka 30 mtu anaishi akikosa vitu muhimu kama:
i-kujiamini,
ii-mwamko,
iii-jitihada,
iv-ubunifu,
v-kujifunza kwa wenzake,
vi-kwenda na wakati na kujua alama za nyakati,
viii-KUMTEGEMEA MWENYEZI NA KUMWAMINI!!!
Matokeo yake anajenga utegemezi kwenye mambo yasiyo kuwa na uhakika wowote sawa na kukalia kuti kavu!
huyu dogo atakua ametumwa na boss wake ambaye hakuweza kufika mahakamani, sidhani kweye umri huu anaweza kuwa ngangari kwenye hii sanaa maana wazungu wanasema the fine wine it get better with age,Huyu bado yosso wataalam wanaingia ndani bila kupitia mlangoni
ReplyDeleteHapa mfano wake ni pale GUTA (Mkokoteni wa magurudumu matatu) wenye uwezo wa kubeba gunia lumbesa 3 tu, UNABEBESHWA MZIGO WA TANI MOJA NA NUSU (GUNIA 15)!
ReplyDeleteMATOKEO YAKE GUTA NA SHEHENA YA MZIGO WAKE LINAKULA MWELEKA HUKU DEREVA AKIWA JUU YAKE CHALI !!!
Hata kama Serikali haiamini na kuendekeza imani za ushirikina lakini imeweka wazi sheria ya kushughulikia masuala ya uchawi – ipo WICHCRAFT ACT(1928) ambayo imeendelea kufanyiwa marekebisho Act No. 12 of 1998. Hivyo mtu anapokuwa na zana zinazotumuka ktk mambo ya kichawi kwa lengo la kuzuia, kuchelewesha, kutisha mtu mwenye wajibu wa kutekeleza majukumu yake rasmi, hata kutishia amani, kusaibisha majeraha, kifo kwa madawa na hirizi basi anakuwa ametenda kosa. Anawezatoozwa faini ama kifungo kisichopungua miaka mitano.
ReplyDeleteLohhh !
ReplyDeleteMgosi Rajabu, kwa msala uliokupata asubuhi ya leo Mahakama ya Kisutu mwombe Ankali Michuzi akutafutie wandugu wa kukupokea Majuu ukaishi huko Sweden ama Norway na ndugu zetu Madiaspora!
(LAKINI UACHE VIFAA VYAKO VYA KAZI USIENDE NAVYO NDUGU ZETU HUKO WAMEKUWA WAZUNGU WATAKUOGOPA KUKUPOKEA KAMA UTAENDA NA FULL NONDOZZZ ZAKO, mapembe ya mbuzi,hirizi,mavumba na masinzi meusi,tunguri,ukucha wa paka,Bundi aliyekuwa hai, shuka ama tambara la kaniki na ngozi nyeusi ya fisi unayovaa kiunoni wakati wa kazi)
Uso hapa Tanzania utauweka wapi?
Muheza-Tanga hakutakalika!
Dar Es Salaam, hakutakalika!
Mdau Anony wa Wed Dec 19, 02:16:00 PM 2012
ReplyDelete...KAMA WEWE NDIO DAKITARI UNAWEZA KWELI KUKOSEA MASHARITI?
Hahahaha ktk umri wake wa miaka 30 ataweza mashariti mengi lakini mawili (2) haya yatakuwa magumu
i-pombe,
ii-mademu,
Inawezekana Dokta. Rajabu Zuberi alikiuka mashariti ya kazi kwa no. (i) ama (ii) hapo juu.
Lohhh ndio maana Uganga wanaweza Wazee !!!
Dokta Rajabu unafahamu ni nini kimekuponza zoezi likakwama?
ReplyDeleteNi hiyo simu ya Mkononi uliyoishika mkono wako wa kulia!
SABABU ZA KISAYANSI NI KUWA MAWIMBI YA MAWASILIANO YAMEINGILIANA KATI YA TEKINOLOJIA MOJA (ya wazi-simu) NA TEKINOLOJIA YA PILI (ya gizani-uchawi),,,HILO NDIO KOSA ULILOFANYA wewe mwenye hadi sasa huko Lupango ulipo bado hujalitambua, HIYO SIMU YA MKONONI NDIO IMEVUJISHA MAWIMBI YA MAWASILIANO HADI UKAONEKANA NA KUKAMATWA, KAMA USINGEKUJA NA SIMU YAKO YA MKONONI HAPO UNGEFANIKISHA!!!
Doktori ulichokosea hadi umebumbulukiwa umelala na kuamka na jasho chafu hukukoga ukaja moja kwa moja 'kazini' hapo Mahakamani Kisutu.
ReplyDeleteNdio maana ngoma imegonga ukuta!
Rajabu Zuberi....kwacha!, kwacha!, kwacha!, kwacha!, kwacha!(Napiga Makopo)
ReplyDeleteMimi ni Babu yako, Profesa wako na Mwalimu wako wa Uganga nikiwa Kijijini-Kerege,Muheza-Tanga, niliona usiku katika TV yetu asilia (mtungi na maji) ya kuwa utakamatwa, nilijaribu kutuma mawasiliano yetu ya Satelaiti asilia lakini mawingu ya mvua yalisumbua netweki ilikuwa mbaya sijakupata hadi alfajiri nalala, ndio nikazinduka nikaona umekamatwa na umewekwa hapo chini ya ulinzi.
SASA HAPA NAKUPA MBINU YA KUCHOMOKA HAPO ULIPOWEKWA UMEKAA, UKAYEYUKA KAMA BARAFU,,,FANYA HIVI:
Jamba kwa mshindo mkubwa kabisa !
UKIFANYA HIVYO TU, KILA MTU HAPO WALIKUZUNGUKA WATACHANGANYIKIWA NA HAWATAKUONA UTAWEZA KUWATOKA UKATOROKA...MOJA KWA MOJA NENDA UBUNGO UKAPANDE BASI UJE KIJIJINI KEREGE, MUHEZA-TANGA, NIJE NIKUPE DOZI YA KUMALIZIA!
MIMI NIMESHA SETI MITAMBO YOTE HUKU KIJIJINI NI WEWE TU MALIZIA ZOEZI HILO KAMA NILIVYO KUELEKEZA!
Je na wale wanaoingia mahakamani wakiwa wamevalia misalaba, rozari, na tasbihi nao wawekwe chini ya ulinzi? Haya ni mambo ya imani. Mwenye imani katika rozari au tasbihi hana tofauti na mwenye imani katika tunguri. AACHIWE, hana kosa lolote.
ReplyDeleteHata kama Serikali haiamini na kuendekeza imani za ushirikina lakini imeweka wazi sheria ya kushughulikia masuala ya uchawi – ipo WICHCRAFT ACT(1928, Cap 18 ambayo imeendelea kufanyiwa marekebisho Act No. 12 of 1998. Hivyo mtu anapokuwa na zana zinazotumuka ktk mambo ya kichawi kwa lengo la kuzuia, kuchelewesha, kutisha mtu mwenye wajibu wa kutekeleza majukumu yake rasmi, hata kutishia amani, kusaibisha majeraha, kifo kwa madawa na hirizi basi anakuwa ametenda kosa. Anawezatoozwa faini ama kifungo kisichopungua miaka mitano.
ReplyDeleteKila kitu sasa kigumu!
ReplyDeleteWajameni tuendeshe maisha kwa kujiamini, kuwa na bidii na kufuata kanuni sheria na taratibu!
Tuache kujenga Mategemeo na matumaini juu ya akina 'Babu' na 'Bibi' kule Vibandani kwa kuwa kama tunavyoona hapa hadi Uchawi unagonga mwamba!