Picture
Na Happy Katabazi.
Mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la RAJABU ZUBERI (30), mkazi wa Kerege, Muheza, Tanga, akiwa chini ya ulinzi wa Wanausalama leo saa mbili asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam, baada kifaa cha upekuzi kumnasa mganga huyo akiwa na vifaa vyake vya uganga ambavyo alikuwa amekuja navyo mahakamani hapo kwa ajili ya kufanyia mambo ya kishirikina katika kesi moja inayomkabili  mmoja wa washtakiwa mahakamani hapo. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Hana hata haya aibu imemjaa asijue la kufanya anaomba ardhi ufunguke azame au uje upepo mkali wenye vumbi atimke,mtoto mdogo bado brazamen wa nguvu unashika na kushiriki mambo ya ajabu namna hiyo, wewe ulisikia wapi mambo haya yanafanikisha ktk vitu vyenye asili ya sayansi.

    ReplyDelete
  2. vifaa vya upekuzi bongo kiboko,mtu anaingia na bastora kwenye ndege havioni lakini Ndumba vinanasa.

    ReplyDelete
  3. Kwani kukamatwa na vitu vya asili au uganga ni kosa kisheria au wana usalama wana mnyanyasa huyu bwana na kama ni kosa je serikali na viungo vyake vinaamini uchawi???!!!

    Akijitetea anadumisha mila zake ni kosa la practise his freedom na kuishi huru na kuamini chochote??? kama sheria zinavyosema??

    Wanasheria tujadili ili swala.

    ReplyDelete
  4. Jamani AIBU sana tu! Unaesema vitu vya asili sio tatizo ni kweli LAKINI ninavyoelewa vitu vya asili huwa havifichwifichwi sasa huyu jamaa angevaa kiasili kabsa tuelewe moja kwamba anadumisha mila.Huu ni uganga wa kienyeji kabsa jamani kijana anaonekana katoka PASINAA kumbee uchawi mtupu lol aibu...!

    ReplyDelete
  5. Mi sielewi,,na sielewi kabisa,,,kwanini mtu huyu adhalilishwe namna hii kwa beliefs zake,,,basi na tuambiwe sasa kama SIRIKALI hii inaamini uchawi,,,hawa askari ingetakiwa wamuweke chini ya ulinzi kama angekua na BOMU au VITU VIZITO mtu huyu na sio matunguli haya na mazagazaga yake,,hii ni KUJIDHALILISHA,,,,na ndo maana hata CNN wametuweka kwenye ranks za juu katika mataifa yanayoamini kupita kiasi katika ushirikina.

    ReplyDelete
  6. Sasa huo uchawi wako mbona haikukusaidia ili usikamatwe?

    ReplyDelete
  7. Hoja ya msingi hapa ni kuangalia iwapo kati ya "hizo zana za jadi" alizokutwa nazo,kuna chochote ambacho kingeweza kuhatarisha usalama na uhai wa watu waliohudhuria ndani ya mahakama?hapa,vitu ninavyo vizungumzia ni kama kitu chochote chenye ncha kali kama kisu,wembe,mshale,panga,mkuki,;silaha kama bastora,bunduki,grenade,bomu,baruti,kisu cha kivita,nk;au maji yenye sumu,acid,harufu mbaya inayodhuru fahamu,nk;na vinginevyo ambavyo ni hatari kwa binadamu.LAKINI,kama vitu alivyokutwa navyo ni haya Mabuyu yetu ya kienyeji,Tunguli,Hirizi,Ngozi ya ng'ombe au kondoo,Jivu,Shanga,Usinga,Pembe za Tunguli,nk.,"huo ni upuuzi mtupu wa kijadi" ambao hautomfanya mhusika kuonekana na "kosa la kutaka kumdhuru mtu!".tafadhali sana,haya ni maoni yangu binafsi!Maana mhusika,anaweza kudai kwamba,yeye Dini yake au Imani yake ya Kidini ni "Imani za Kijadi",na kwamba,aliamini kwa kuwa na zana zile,angeweza "Kuiomba Miungu Wake",wamsamehe "mtuhumiwa mahakamani aliyemkusudia KUMSAIDIA ILI ASAMEHEWE NA MAHAKAMA",kwa imani na nia njema kabisa za kumsaidia mtuhumiwa "kama vile Wakili au Advocate atakavyo fanya akikusudia kumsaidia mtuhumiwa aepuke hukumu ya mahakama"(the same analogy)! simple analysis! hapo je,wadau? mwachieni huyo jamaa aende zake,bali,atahitaji elimu kidogo!

    ReplyDelete
  8. Serikali haina dini na haiamini uchawi mwachilieni dogo mara moja na sayansi yake asilia...ebo!!!!!!
    KITAMBI NOMA-ARUSHA

    ReplyDelete
  9. aachiwe MGANGA auwawe RAMA JANGILI

    ReplyDelete
  10. KAMA SERIKALI YETU INAAMINI HAYA MAMBO BASI NA HII SERIKALI ITAKUWA HAZIMO

    HUYU MTU NIWAKUACHIWA HURU NA SIO KUMUWEKA CHINI YA ULINZI WA ASKARI HIVI HII INAMAANISHA KWENYE MZUNGUKO WOTE WA SERIKALI INAAMINI HAYA MAMBO NA WANAYAFANYA NA WAO NDIO MAANA WAKAYAOGOPA HAYA MASUALA

    SERIKALI IJIANGALIE NA WANACHOKIFANYA, ISIWE SERIKALI YA ABUNUWASI

    ReplyDelete
  11. Duhhh ama kweli mambo ni magumu siku hizi!

    Yaani hata mbinu za Ufundi zinakwama?

    TUKIO HILI LITAWAKOSESHA SANA MAPATO YA WEEK END 'MABABU' WANAOTEMBELEWA NA WATEJA WAO KILA MWISHO WA WIKI BAADA YA WATEJA KUDHIHIRISHA KWA KUONA YA KUWA MAMBO YANAKWAMA!

    ReplyDelete
  12. Yaani hawa askari hawana cha kufanya? Tatizo ni kwamba watu wengi wanaamini mauchawi, wasingaamini haya mambo wangecheka na kumfukuzilia mbali huyu mtu aondoke mahakamani. Haya madunguli hayawezi kubadilisha kesi ya huyo mshatikiwa kamwe. Inabidi nchi yetu iamke uchawi haupo tusipoteze muda na pesa kwa imani potovu!

    ReplyDelete
  13. Jamani elimu ni muhimu sana!

    ReplyDelete
  14. UWEZO WA MWENYEZI UPO JUU MNO KULIKO NGUVU ZA UCHAWI !

    Bwana Mdogo Dakta Rajas na mamia kwa maelfu ya Babu zako Madakitari wenzio mmethibitisha hilo kwa matokeo ya zoezi lako kushindwa vilivyo hii leo asubuhi!

    MGOSI UMEUMBUKA NA UMETUANGUSHA SANA KTK UMRI HUO KUSHIRIKI VITU HIVYO, PIA TUNASHUKURU SANA LIMEKUWA NI FUNDISHO KWA WENGINE!

    LEO HII SAA 2:00 ASUBUHI MCHANA KWEUPE (wala sio usiku wa giza) HAPO MAHAKAMANI KISUTU WEWE MWENYEWE UMETHIBITISHA MGOSI RAJABU ukishuhudia BUNDI akikufia mikononi na usijue la kufanya!

    Zoezi limekwama, BUNDI uliyetaka kumrusha kimya kimya hapo Mahakamani ndio kwanza kakufia mikononi!

    KWA USANII WENU NA UTAALAMU WENU WA KUBAHATISHA NA KUSIKILIZIA MATOKEO ENDAPO:

    1.ZOEZI LINGEFANIKIWA:
    Mganga ungejisifu kuwa wewe ni bingwa.

    2.ZOEZI LINGEKWAMA:
    Mganga ungemlaumu Mteja ya kuwa amekosea Mashariti ama amekiuka Mashariti, SASA IMETOKEA WEWE MWENYEWE BUNDI AMEKUFIA MIKONONI (SIO MTEJA WAKO), SASA JE UTADAI NINI?, KAMA WEWE NDIO DAKITARI UNAWEZA KWELI KUKOSEA MASHARITI?

    ReplyDelete
  15. NI UAMUZI WA BUSARA SERIKALI HASA YA TZ KUZINGATIA KUWA HAINA IBARA ZA SAYANSI KAMA HIZI.

    NI VILE MARA ZOTE NI ZA KUBAHATISHA NA PATA POTEA!

    KAMA DOGO RAJA ALIVYOKWAMA LEO ASUBUHI MAHAKAMANI KISUTU.

    ReplyDelete
  16. Kwa kuwa Mahakama ni ya watu ina Sauti na sauti ya watu ni sauti ya Mwenyezi Mungu!

    Kwa matokeo ya kushindikana kwa zoezi lako la kumchinja paka (ukifikiri huonekani) ukiwasaidia Wateja wako (Wahalifu) ILI KUIPINDISHA SHERIA NA MAAMUZI YA MAHAKAMA ni wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu AMEKATAA KATA KATA!

    ReplyDelete
  17. Hapo ndio tunashuhudia mambo mawili (2):

    1.Dakitari akifariki yeye mwenyewe mbele ya mgonjwa wake aliyekuwa mahututi hajitambui akibaki hai!

    2.Punda akifa na mzigo mgongoni!

    ReplyDelete
  18. MGOSI RAJABU ZUBERI,

    HUWEZI KUWA NA UJASIRI WA KUISHI MAISHA YA WAZI NCHINI KWA AIBU HII ILIYOKUKUTA,

    ITABIDI UHAMIE NCHI ZINGINE UKAISHI,

    NAKUSHAURI HIVI:

    CHUKUA PICHA HII PAMOJA NA RB YA POLISI KWA KISA HIKI UENDE UBALOZI WA MAREKANI UKAOMBE VIZA YA KUPEWA HIFADHI ILI UKAISHI HUKO, KWA KUEPUKA JAMII NA USHAMBULIZI KWA TUHUMA ZA UCHAWI!!!

    ReplyDelete
  19. KIZA KIMETANDA, MATUMAINI MAKUBWA TULIYOYAWEKA KWA WAGANGA YAMEPOTEA!

    Tunashauriwa tuachane na Ushirikina, tuanze mwaka mpya 2013 kwa staili mpya.

    Hii ni SALAMU YA KRISMASI na MWAKA MPYA!

    ReplyDelete
  20. Hili ni janga la Taifa!

    Katika umri mdogo wa miaka 30 mtu anaishi akikosa vitu muhimu kama:

    i-kujiamini,
    ii-mwamko,
    iii-jitihada,
    iv-ubunifu,
    v-kujifunza kwa wenzake,
    vi-kwenda na wakati na kujua alama za nyakati,
    viii-KUMTEGEMEA MWENYEZI NA KUMWAMINI!!!

    Matokeo yake anajenga utegemezi kwenye mambo yasiyo kuwa na uhakika wowote sawa na kukalia kuti kavu!

    ReplyDelete
  21. huyu dogo atakua ametumwa na boss wake ambaye hakuweza kufika mahakamani, sidhani kweye umri huu anaweza kuwa ngangari kwenye hii sanaa maana wazungu wanasema the fine wine it get better with age,Huyu bado yosso wataalam wanaingia ndani bila kupitia mlangoni

    ReplyDelete
  22. Hapa mfano wake ni pale GUTA (Mkokoteni wa magurudumu matatu) wenye uwezo wa kubeba gunia lumbesa 3 tu, UNABEBESHWA MZIGO WA TANI MOJA NA NUSU (GUNIA 15)!

    MATOKEO YAKE GUTA NA SHEHENA YA MZIGO WAKE LINAKULA MWELEKA HUKU DEREVA AKIWA JUU YAKE CHALI !!!

    ReplyDelete
  23. Hata kama Serikali haiamini na kuendekeza imani za ushirikina lakini imeweka wazi sheria ya kushughulikia masuala ya uchawi – ipo WICHCRAFT ACT(1928) ambayo imeendelea kufanyiwa marekebisho Act No. 12 of 1998. Hivyo mtu anapokuwa na zana zinazotumuka ktk mambo ya kichawi kwa lengo la kuzuia, kuchelewesha, kutisha mtu mwenye wajibu wa kutekeleza majukumu yake rasmi, hata kutishia amani, kusaibisha majeraha, kifo kwa madawa na hirizi basi anakuwa ametenda kosa. Anawezatoozwa faini ama kifungo kisichopungua miaka mitano.

    ReplyDelete
  24. Lohhh !

    Mgosi Rajabu, kwa msala uliokupata asubuhi ya leo Mahakama ya Kisutu mwombe Ankali Michuzi akutafutie wandugu wa kukupokea Majuu ukaishi huko Sweden ama Norway na ndugu zetu Madiaspora!

    (LAKINI UACHE VIFAA VYAKO VYA KAZI USIENDE NAVYO NDUGU ZETU HUKO WAMEKUWA WAZUNGU WATAKUOGOPA KUKUPOKEA KAMA UTAENDA NA FULL NONDOZZZ ZAKO, mapembe ya mbuzi,hirizi,mavumba na masinzi meusi,tunguri,ukucha wa paka,Bundi aliyekuwa hai, shuka ama tambara la kaniki na ngozi nyeusi ya fisi unayovaa kiunoni wakati wa kazi)

    Uso hapa Tanzania utauweka wapi?

    Muheza-Tanga hakutakalika!
    Dar Es Salaam, hakutakalika!

    ReplyDelete
  25. Mdau Anony wa Wed Dec 19, 02:16:00 PM 2012

    ...KAMA WEWE NDIO DAKITARI UNAWEZA KWELI KUKOSEA MASHARITI?

    Hahahaha ktk umri wake wa miaka 30 ataweza mashariti mengi lakini mawili (2) haya yatakuwa magumu

    i-pombe,
    ii-mademu,

    Inawezekana Dokta. Rajabu Zuberi alikiuka mashariti ya kazi kwa no. (i) ama (ii) hapo juu.

    Lohhh ndio maana Uganga wanaweza Wazee !!!

    ReplyDelete
  26. Dokta Rajabu unafahamu ni nini kimekuponza zoezi likakwama?

    Ni hiyo simu ya Mkononi uliyoishika mkono wako wa kulia!

    SABABU ZA KISAYANSI NI KUWA MAWIMBI YA MAWASILIANO YAMEINGILIANA KATI YA TEKINOLOJIA MOJA (ya wazi-simu) NA TEKINOLOJIA YA PILI (ya gizani-uchawi),,,HILO NDIO KOSA ULILOFANYA wewe mwenye hadi sasa huko Lupango ulipo bado hujalitambua, HIYO SIMU YA MKONONI NDIO IMEVUJISHA MAWIMBI YA MAWASILIANO HADI UKAONEKANA NA KUKAMATWA, KAMA USINGEKUJA NA SIMU YAKO YA MKONONI HAPO UNGEFANIKISHA!!!

    ReplyDelete
  27. Doktori ulichokosea hadi umebumbulukiwa umelala na kuamka na jasho chafu hukukoga ukaja moja kwa moja 'kazini' hapo Mahakamani Kisutu.

    Ndio maana ngoma imegonga ukuta!

    ReplyDelete
  28. Rajabu Zuberi....kwacha!, kwacha!, kwacha!, kwacha!, kwacha!(Napiga Makopo)

    Mimi ni Babu yako, Profesa wako na Mwalimu wako wa Uganga nikiwa Kijijini-Kerege,Muheza-Tanga, niliona usiku katika TV yetu asilia (mtungi na maji) ya kuwa utakamatwa, nilijaribu kutuma mawasiliano yetu ya Satelaiti asilia lakini mawingu ya mvua yalisumbua netweki ilikuwa mbaya sijakupata hadi alfajiri nalala, ndio nikazinduka nikaona umekamatwa na umewekwa hapo chini ya ulinzi.

    SASA HAPA NAKUPA MBINU YA KUCHOMOKA HAPO ULIPOWEKWA UMEKAA, UKAYEYUKA KAMA BARAFU,,,FANYA HIVI:

    Jamba kwa mshindo mkubwa kabisa !

    UKIFANYA HIVYO TU, KILA MTU HAPO WALIKUZUNGUKA WATACHANGANYIKIWA NA HAWATAKUONA UTAWEZA KUWATOKA UKATOROKA...MOJA KWA MOJA NENDA UBUNGO UKAPANDE BASI UJE KIJIJINI KEREGE, MUHEZA-TANGA, NIJE NIKUPE DOZI YA KUMALIZIA!

    MIMI NIMESHA SETI MITAMBO YOTE HUKU KIJIJINI NI WEWE TU MALIZIA ZOEZI HILO KAMA NILIVYO KUELEKEZA!

    ReplyDelete
  29. Je na wale wanaoingia mahakamani wakiwa wamevalia misalaba, rozari, na tasbihi nao wawekwe chini ya ulinzi? Haya ni mambo ya imani. Mwenye imani katika rozari au tasbihi hana tofauti na mwenye imani katika tunguri. AACHIWE, hana kosa lolote.

    ReplyDelete
  30. Hata kama Serikali haiamini na kuendekeza imani za ushirikina lakini imeweka wazi sheria ya kushughulikia masuala ya uchawi – ipo WICHCRAFT ACT(1928, Cap 18 ambayo imeendelea kufanyiwa marekebisho Act No. 12 of 1998. Hivyo mtu anapokuwa na zana zinazotumuka ktk mambo ya kichawi kwa lengo la kuzuia, kuchelewesha, kutisha mtu mwenye wajibu wa kutekeleza majukumu yake rasmi, hata kutishia amani, kusaibisha majeraha, kifo kwa madawa na hirizi basi anakuwa ametenda kosa. Anawezatoozwa faini ama kifungo kisichopungua miaka mitano.

    ReplyDelete
  31. Kila kitu sasa kigumu!

    Wajameni tuendeshe maisha kwa kujiamini, kuwa na bidii na kufuata kanuni sheria na taratibu!

    Tuache kujenga Mategemeo na matumaini juu ya akina 'Babu' na 'Bibi' kule Vibandani kwa kuwa kama tunavyoona hapa hadi Uchawi unagonga mwamba!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...