Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo jioni alijumuika na mamia ya wakazi wa mji wa Bagamoyo katika mazishi ya alhaji Shekhe Abdallah Masoud Jembe, mmoja wa mashekhe maarufu na mzee wa mji wa Bagamoyo.Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Mwenyekiti wa Chama cha upinzani cha CUF prof.Ibrahim Lipumba ni miongoni wa viongozi waliohudhuria mazishi hayo.Pichani Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na makamu wa Rais Dkt.Momahed Gharib Biala wakiweka udongo katika kaburi la Marehemu Shekhe Abdallah Masoud Jembe wakati wa mazishi yaliyofanyika mjini Bagamoyo leo jioni
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka Udongo Kaburini.
Makamu wa Rais,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akiweka Udongo Kaburini wakati wa Mazishi ya Alhaji Shekhe Abdallah Masoud Jembe.
Mashallah rais wetu akuzidishie inshallah
ReplyDeleteMwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi
ReplyDeleteJK ni mtu wa watu,mwenyezi mungu akujaalie kila la kheri,mwenyezi mungu amlaze mahali pema Alhaj Sheikh Jembe.
ReplyDelete