Na Thehabari.com 
 VYOMBO vya habari nchi vimeombwa kutoa elimu kwa jamii juu ya manufaa ya iwepo wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (National ICT Broadband Backbone-NICTBB) ili wananchi wauelewe na kuulinda kutokana na umuhimu wake. 
 Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Uendeshaji wa NICTBB, Adin Mgendi alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo anuai vya habari juu ya utendaji kazi wa mkongo huo na manufaa yake kwa taifa. 
 Mgendi alisema manufaa ya ujenzi wa Mkongo wa mawasiliano nchini yameanza kujitokeza hivyo Watanzania wana kila sababu ya kuulinda mtandao huo kwani unaumuhi mkubwa kwa jamii na taifa. Alisema kwa sasa jumla ya nchi sita, ambazo ni pamoja na Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya zimeunganishwa na Tanzania hivyo nchi yetu ikibeba dhamana ya kuwahudumia kupitia mtandao wa Mkongo. 
 Mtalamu huyo alivitaka vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa wananchi hasa waliopo karibu na njia ya mkongo ili wasiuharibu kupitia shughuli mbalimbali za kijamii zinazofanyika ardhini. 
 Akifafanua zaidi kwa wahariri wao, Ofisa Biashara wa Mkongo, Thomas Lemunge alisema kwa sasa mikoa yote ya Tanzania Bara tayari imeunganishwa na mkongo hivyo kurahisisha miundobinu ya mawasiliano.
 Aidha aliongeza kuwa mtandao wa mkongo ambao ujenzi wake uaendelea umepita maeneo anuai; ikiwemo ardhini pembezoni mwa barabara, mashambani, juu ya nyaya za umeme na kwenye maji huku ukiwa na mizunguko mitatu yaani wa Kaskazini, Magharibi na Kusini. 
 Awali akizungumza na washiriki hao, kabla ya kufungua warsha hiyo, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini (TEHAMA), Mhandisi Zaipuna Yonah alisema mkongo unamanufaa makubwa kwani hadi sasa matumizi ya intaneti yameongezeka tofauti na awali.
 "Ongezeko la matumizi na faida za mkongo zinaongezeka siku hadi siku na hivyo kukidhi matarajio ya Serikali ya kuziba pengo la matumizi ya TEHAMA kwa wananchi katika maeneo ya mbalimbali ya nchi yetu na hatimaye kukuza uchumi," alisema Yonah. 
Wahariri hao walipata fursa ya kutembelea kituo kikuu kinachoratibu shughuli za mkongo maeneo mbalimbali ya nchi na kuona namna wataalamu wanavyofanya kazi eneo hilo. 
 Mkongo wa taifa ambao kwa sasa unategemewa na nchi jirani za Tanzania na makampuni binafsi katika usabazaji huduma za mawasiliano unasimamiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) huku wakiwa ndio meneja wa Mkongo huo.
 Wahariri wakiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
 Mhariri Mkuu wa Tanzania Daima Bw Ansbert Ngurumo akiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
 Wahariri wakibadilishana mawazo wakati wa mapunziko ya semina hiyo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo
 Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
 Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
Meneja mwendeshaji wa mkongo wa Taifa Bw Adin Mgendi akifafanua jambo
0
Mhandisi wa Mkongo wa Taifa Bw Nsaji Mwamukonda akionesha kwa wahariri aina ya waya unaobeba mkongo huo. Taarifa kamili  ya semina hii badae kidooogo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ni kweli mkngo wa taifa uo na unafanya kazi lakini je bei ya internet bundle bado kubwa sana sana jamani nchi zilizo endelea wameona ni bora kushusha garama ya mawasiliano ambayo ni muhimu kwa kila mtu kuliko kulazimisha bei kubwa ikiwezekana kila mtandao wa simu ungerusiwa kua na mkongo wake kama Kenya wanyao mitatu sasa

    ReplyDelete
  2. mkongo ni kitu gn?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...