Na Thehabari.com
VYOMBO vya habari nchi vimeombwa kutoa elimu kwa jamii
juu ya manufaa ya iwepo wa Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano (National ICT Broadband Backbone-NICTBB)
ili wananchi wauelewe na kuulinda kutokana na umuhimu
wake.
Changamoto hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na
Meneja Uendeshaji wa NICTBB, Adin Mgendi alipokuwa
akizungumza na wahariri wa vyombo anuai vya habari juu
ya utendaji kazi wa mkongo huo na manufaa yake kwa
taifa.
Mgendi alisema manufaa ya ujenzi wa Mkongo wa
mawasiliano nchini yameanza kujitokeza hivyo
Watanzania wana kila sababu ya kuulinda mtandao huo
kwani unaumuhi mkubwa kwa jamii na taifa.
Alisema kwa sasa jumla ya nchi sita, ambazo ni pamoja
na Malawi, Zambia, Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya
zimeunganishwa na Tanzania hivyo nchi yetu ikibeba
dhamana ya kuwahudumia kupitia mtandao wa Mkongo.
Mtalamu huyo alivitaka vyombo vya habari kuendelea
kutoa elimu kwa wananchi hasa waliopo karibu na njia
ya mkongo ili wasiuharibu kupitia shughuli mbalimbali
za kijamii zinazofanyika ardhini.
Akifafanua zaidi kwa wahariri wao, Ofisa Biashara wa
Mkongo, Thomas Lemunge alisema kwa sasa mikoa yote ya
Tanzania Bara tayari imeunganishwa na mkongo hivyo
kurahisisha miundobinu ya mawasiliano.
Aidha aliongeza kuwa mtandao wa mkongo ambao ujenzi
wake uaendelea umepita maeneo anuai; ikiwemo ardhini
pembezoni mwa barabara, mashambani, juu ya nyaya za
umeme na kwenye maji huku ukiwa na mizunguko mitatu
yaani wa Kaskazini, Magharibi na Kusini.
Awali akizungumza na washiriki hao, kabla ya kufungua
warsha hiyo, Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano nchini (TEHAMA), Mhandisi Zaipuna Yonah
alisema mkongo unamanufaa makubwa kwani hadi sasa
matumizi ya intaneti yameongezeka tofauti na awali.
"Ongezeko la matumizi na faida za mkongo zinaongezeka
siku hadi siku na hivyo kukidhi matarajio ya Serikali
ya kuziba pengo la matumizi ya TEHAMA kwa wananchi
katika maeneo ya mbalimbali ya nchi yetu na hatimaye
kukuza uchumi," alisema Yonah.
Wahariri hao walipata fursa ya kutembelea kituo kikuu
kinachoratibu shughuli za mkongo maeneo mbalimbali ya
nchi na kuona namna wataalamu wanavyofanya kazi eneo
hilo.
Mkongo wa taifa ambao kwa sasa unategemewa na nchi
jirani za Tanzania na makampuni binafsi katika
usabazaji huduma za mawasiliano unasimamiwa na Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) huku wakiwa ndio meneja wa
Mkongo huo.
Wahariri wakiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
Mhariri Mkuu wa Tanzania Daima Bw Ansbert Ngurumo akiangalia waya wa Mkongo wa Taifa
Wahariri wakibadilishana mawazo wakati wa mapunziko ya semina hiyo katika hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo
Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
Afisa biashara wa Mkongo wa Taifa Bw. Thomas Lemunge akielezea faida za huduma hiyo katika mawasiliano ya tehama
![]() |
Meneja mwendeshaji wa mkongo wa Taifa Bw Adin Mgendi akifafanua jambo |
0
Mhandisi wa Mkongo wa Taifa Bw Nsaji Mwamukonda akionesha kwa wahariri aina ya waya unaobeba mkongo huo. Taarifa kamili ya semina hii badae kidooogo...
ni kweli mkngo wa taifa uo na unafanya kazi lakini je bei ya internet bundle bado kubwa sana sana jamani nchi zilizo endelea wameona ni bora kushusha garama ya mawasiliano ambayo ni muhimu kwa kila mtu kuliko kulazimisha bei kubwa ikiwezekana kila mtandao wa simu ungerusiwa kua na mkongo wake kama Kenya wanyao mitatu sasa
ReplyDeletemkongo ni kitu gn?
ReplyDelete