Meli ya kivita  ya kupambana na uharamia aina ya  Anti Submarine iitwayo  Marshal Shaposhnikov’,  ilipokuwa ikiingia na kasha baadae kutia nanga katika bandari ya Dar es Salaam, kwa ziara fupi yenye lengo la kuimarisha urafiki baina ya Jeshi la Wanamaji wa Tanzania na Urusi. Wakati nchi ya Somalia ikiendelea kuwa kitovu cha uharamia, jumuiya ya kimataifa ilikubaliana kudhamiria kupambana na vitendo hivyo viovu. Lakini hadi sasa, wakati nchi nyingine zikitumia mbinu mbalimbali katika mapambano hayo, ni nchi za Russia, India na China pekee zinazosindikiza meli zao za biashara na nyinginezo ili kuzilinda na uharamia. Meli hiyo imewasili siku ya Jumamosi na inategemea kuondoka kesho, Jumatano.
Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh  akiambatana na kiongozi wa wanajeshi waliofatana na meli hiyo Rear Admiral Vdovenko
Kwa pamoja, Balozi Rannikh na wanajeshi wa Kirusi waliimba wimbo wao wataifa wakiwa katika meli.
Balozi Rannikh akiwapongeza wanajeshi wake kwa kufika Dar es Salaam, Tanzania na kuwakaribisha nchi pia.
Baada ya salamu hizo, Balozi Rannikh nae alikaribishwa keki na mmvinyo iliyoandaliwa na wanajeshi katika meli.
Balozi wa  Urusi hapa nchini Mheshimiwa Alexander Rannikh akipokea salamu kutoka kwa  kiongozi mkuu Rear Admiral Vladimir Vdovenko wakati alipotembelea meli hiyo bandarini.

Wanajeshi wa Kirusi wakionesha umahili wao wa ukakamavu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Warusi hawa hakuna cha keki na mvinyo, hiyo ni vodka kavukavu mchana mchana, watu na tamaduni zao.

    ReplyDelete
  2. Mrusi huyu,hakuna cha mvinyo hapa,jamaa anapata vodka kavukavu mchana mchana, dumisha tamaduni rafiki.

    ReplyDelete
  3. Hehehehe Wadau hapo juu,

    Hiyo Keki ni zuga zuga tu kama chachandu tu msije Watanzania mkaanza kulalamika ohhh Warusi wamekuja Kijeshi Tanzania wanalewa tu,

    Hawa Warusi si wanatujua Watanzania kwa lawama?

    Mambo hapo ni mpango mzima maji ya betriii!!!

    ReplyDelete
  4. hawajama wakofiti mbaya, hakunamwenyemimba hapo... embu uje ucheki wanajeshi wetu kati ya kumi watatu wana mimba. lol

    Mimba (Kitambi)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...