Flashback: Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Mwanaidi Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho wa Balozi wetu huyo nchini humo tarehe 16.09.2010


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.

Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni:-

1.           Bw. Dushhood M. K. Mndeme
2.           Mhe. Balozi Abdi Mshangama
3.           Mhe. Dkt. Leonidas Mushokolwa
4.           Mhe. Dkt. Harold Utouh
5.           Mhe. Saidi Mtanda (Mb.)
6.           Mhe. Betty Machangu (Mb.)
7.           Bw. Affan Othman Maalim
8.           Bw. Abdurahaman Abdallah

Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 22 Januari, 2013 hadi tarehe 21 Januari, 2016.
  
IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA

USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

15 FEBRUARI, 2013






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mdau wa kwanza km umeumia kunywa sumu

    ReplyDelete
  2. acha upuuzi anony wa kwanza(mon feb 18, 03:40pm2013)

    ReplyDelete
  3. Huyo bwege wa Kanza alikuwa analalamikia Udini kutumika ktk Uteuzi huu sijui kwa Kigezo gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...