Mshindi wa tano wa DStv Rewards, Alphonce Mlekwa Omary
(wa pili kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko
wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu(kushoto), Meneja Mahusiano wa
MultiChoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kutoka kulia) na Meneja
Muajiri wa MultiChoice Tanzania, Tike Mwakitwange(kulia), mara ya
kukabidhiwa mfano wa hundi ya Tshs Milioni 5 kuashiria ushindi alioibuka
nao.
Wateja wa DStv ambao wanalipia malipo ya mwezi ya
akaunti zao kabla ya kukatika wanaendelea kubahatika na kuibuka washindi
wa mamilioni ya pesa kila wiki. Hiyo ni kupitia droo maalumu ya DStv
ambayo imepewa jina la DStv Rewards.
Mteja ambaye amebahatika kuibuka na kitita cha Tshs Milioni 5 wiki hii na hivyo kuifanya idadi ya washindi kufikia watano ni Bw. Alphonce Mlekwa Omary.
Tabasamu
la ushindi. Ndivyo inavyoonekana katika picha kwa mshindi wa 5 wa DStv
Rewards akifurahia kitita cha Tshs 5,000,000. Waliomzunguka pembeni ni
ndugu zake ambao walimsindikiza na kufurahia pamoja naye ushindi.
Duuuu Multi Choice, Ma-meneja wenu mbona mademu wazuri zuri tuu, hakuna ma-meneja wanaume? tehee teehe teehee. Wazuri hao acha tuu.
ReplyDelete