Pichani ndio matundu ya risasi zilivyorindima kwenye kioo cha dereva (risasi tatu) na kushoto risasi moja kama kionekanavyo kioo cha juu,mara majambazi hayo kufanikiwa kumjeruhi dereva sehemu ya bega na kufanikiwa kunyakua begi linalosadikiwa kuwa,lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 na kutokomea nazo.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.
Pichani kulia ni Askari Usalama barabarani akichukuliwa maelezo yake kutokana kushuhudia tukio la ujambazi lililofanyika maeneo ya Sayansi mataa-Kijitonyama jijini Dar mapema leo mnamo majira ya saa tano kasoro.
Ambapo kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio
wanaeleza kuwa majambazi hao walikuwa wapatao wanne wakiwa wamepanda
piki piki,ghafla wakasimama na kulizunguka gari aina Vitz yenye usajili
wa namba T929 CCX (pichani chini) kwa haraka,mmoja wao akiwa na mashine
gun na wengine walikuwa na bastola.
Mmoja wao alifyatua risasi hewani
kumtaka dereva asimame na ashushe vioo vya gari yake,kufuatia hali ya
utata wa majibishano ya muda mfupi majambazi hao waliifyatulia risasi
kadhaa gari hiyo upande wa dereva, bahati mbaya wakamjeruhi sehemu
ya bega,ndipo wakafanikiwa kuondoka na begi kubwa linalosadikiwa kuwa
lilikuwa na kiasi cha fedha shilingi milioni 40 (kwa mujibu wa dereva
aliempeleka majeruhi hospitali),mara baada ya majambazi hayo kutimka
wasamalia wema wakamchukua dereva huyo aliyekuwa akigugumia kwa maumivu
ya jeraha lake na kumtafutia tax na hatimae kumkimbiza hospitali ya
Kairuki kwa huduma ya haraka.
Baadhi ya watu wakijaribu kubadilshana mawazo kwa kulitafakari tukio hilo la ujambazi.
Gari iliyokuwa imevamiwa na majambazi ikikokotwa na gari la polisi mara baada ya kushindwa kuwaka.
nadhani hizo pesa zimekuwa raced pahala si bure check ramani ilipotoka hizo pesa mpaka anakoelekea kwani walijuaje kuwa hilo gai lina pesa hicho?
ReplyDeleteHakuna tofauti kati ya ile issue ya Ada Estate wachina walipoibiwa mshahara wa wafanyakazi hao...
walipewa mchoro tu
ReplyDeleteMhmmmmm si bure huo mchongo wa watu wa macounter benki jamaa akichukua wanaripoti na watakuwa na watu wao walioko karibu na hapo wanashutuliwa!! wazeni mbali jamani mambo yamekuwa mabaya sio mpaka mtu wa nje.
ReplyDeleteMtu keshauza lada hapa.
ReplyDeleteInatisha. Namna hii tutafika kweli jamani?
ReplyDeleteKuna haja ya wizara husika kuangalia namba ya kuwa na mashine za wafanyabiashara kupokea na kufanya malipo kwa soft-money. Hapa Africa ya kusini unaweza kuishi mwezi mzima bila kuiona noti na ukalipa kwa kadi ya benki,hii inapunguza sana mambo ya kuuana kwa ajili ya pesa na pengine hata siyo pesa zako mwenyewe. Hii itasaidia, mfano ukiwa na eldu 5 au 20 tu za matumizi nani ataharibu risasi zake kwa hela hiyo,sana sana vibaka watachukua,utasikitika ndio lakini utakuwa salama.
ReplyDeleteWe need to arm all of the police men with hand guns ,if this trooper had a hand gun with him he would have fought back and serve the victim
ReplyDeleteWatu sasa waache kubeba cash kubwakubwa kama hizi watumie transfer za kibenki itapunguza sana matukio kama haya. Inasikitisha sana.
ReplyDeletehilo dili
ReplyDeleteKweli Tanzania si mahali pa kuishi. It's all inside job. Kila mtu mtu anataka kutajirika hata kwa kutoa mtu roho.
ReplyDeleteDuh, tz tulipofikia? Kuna haja ya kuwa na cctv kwenye mataa.. Poor him...
ReplyDeletekiukweli njaa itatuumiza tisipoangalia. Huu mchongo umefanywa na mtu wa karibu au pesa zilipochukuliwa maana siku hizi watu wa mabenki wanamitandao yao wakijua unachukua pesa nyingi wanapanga mikakati. enyi wafanyakazi wataasisi za fedha kuweni na maadili kumbukeni unachofanya leo kwa mwenzio kesho kwako au kwa ndugu yako wa karibu. Polisi waanzie pale pesa zilipotoka.
ReplyDeleteKama hilo gari limetokea bank hiyo bank ishikwe shati kabisaa. Vitendo kama hivi vimekuwa vikitokea sana wafanyabiashara wanapotoka bank!! Inabidi serikali imyaanya'anye leseni hizo bank husika kabisa!!! lazima hiyo ni inside job mia ya mia!
ReplyDeleteUchunguzi ni lazima uanzie hukoooooo bank!! Or huyu mtu hakutokea bank??? Or ni deal limekwenda vibaya
ReplyDeleteWazee wa kazi wamechukua chao. Inabidi sasa jamii ibadilike hatuwezi kuendelea kutembea na magunia ya noti lazima tupate njia mbadala ya malipo.
ReplyDeleteso sad jamani
ReplyDeleteinabidi iitwe FBI hapa kufanya uvhunguzi.
ReplyDelete