CAREERS IN AFRICA INAWATANGAZIA WALE WOTE WENYE SHAUKU YA KUTAFUTA KAZI BARA LA AFRIKA KUHUDHURIA KONGAMANO KUBWA LA KAZI LITAKALOFANYIKA JIJI LA LONDON KUANZIA TAREHE 17 MPAKA 19 MEI , 2013.

CCM UK -TUNAOMBA KUWATANGAZIA WATANZANIA WOTE, BILA YA KUJALI ITIKADI ZAO ZA KISIASA, KUJIANDIKISHA NA KUHUDHURIA KWA WINGI KONGAMANO HILI KWA KUJITAFUTIA AJIRA, AMA HATA KUJIFUNZA MENGI MAZURI YATAKAYOJIRI.

KWA MAELEZO ZAIDI NA JINSI YA KUJIANDIKISHA TAFADHALI TEMBELEA TOVUTI YA: www.careersinafrica.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2013

    Sasa hawa jamaa walihama Afrika sasa kazi za huko za nini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2013

    Janja ya Nyani kwisa jua eee?

    Mzungu ana akili sana, ameona Mwafrika anahangaika kwenda Ulaya anafika Ulaya Uchumi wenyewe umeyumba, anakosa Ajira anakaa Mtaani anakuwa Muhalifu!

    Mzungu amepiga akili anaona aanzishe Careers Africa ili aweze kuwafanya WABEBA MABOX kufungasha virago kurudi kwao kwa kuwa Ulaya haina kazi sasa kazi zipo Africa!

    Breki ya kwanza ni Malampaka,Kwimba na Newala TANZANIA.

    Kazi kwenu akina Mbonde na Maganga safari ya Bongo imewadia!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 17, 2013

    ECONOMIC CHANGES:

    Upepo wa Uchumi hubadilika na muda, inakuwa kama siku hazigandi.

    Miaka ya nyuma, watu walikuwa wanakwenda Zambia na Kenya kuagiza bidhaa kama NGUO NA VIATU lakini sasa hakuna anayekwenda nchi hizo kwa kusaka bidhaa hizo tena.

    Miaka iliyopita watu walikuwa wanaenda Majuu (Waafrica) lakini sasa (Wazungu) ndio wanaokuja kukaa na kutafuta Aafrica!

    Juzi tu palionekana mtiririko wa Wazungu kibao kutoka sio Ugiriki na Ureno kulikofilisika wengine wametokea nchi kama Ujerumani, Uholanzi, Italy ,Marekani na Uswisi kuja kiutafuta maisha, Utajiri na kuwekeza Africa!

    HAYA SASA MNAOBISHA HABARI NDIYO HIYO KAZI KWENU!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 17, 2013

    Haya Wabeba Mabox Majuu safari ya kurudi Bongo Jambaland ndio hiyo sasa!

    Mzungu Mafia sana, amewasukia bonge la mpango.

    Ile puuu unajikuta upo Kijijini kwako (TZ) huku ukiwa huwezi kurudi tena Majuu.

    Si mlikuwa wabishi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 17, 2013

    kikili kikili unasajili (careersinafrica) unajikuta upo volunteer ktk Mradi wa Ukimwi Dar live Mbagala, Darisalama Tanzania,

    mwanawane mkisikia TKO (Technical Knock out) ndio hiyooo Donald Mkameruni amewachapa!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 17, 2013

    Mnaokataa kurudi Bongo mmeona 'mnemba' huo?

    Wasiwasi wangu ni kuwa wewe unakataa kurudi Bongo, unakuja na huo Mpango unapangiwa Kilwa ktk Mradi wa Gesi unafika unakuta Bomba la Gesi linapita Shambani kwenu kuleee Kijijini huku wewe ulipoondoka shamba limeuzwa kwa Wawekezaji (ukapoteza haki zako) na sasa umekuja kama Kibarua wa Mradi.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 17, 2013

    Hiyo ni

    Kutoka YUKEI hadi TANDAHIMBA-NEWALA, MAHUTA /SHIMONI, NEWALA !!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 17, 2013

    Mkubwa ni Mkubwa hata akiwa Mlevi!

    Mwingereza amefanya Utafiti amekuta Jakaya Kiwete amepoteza nguvu kazi kubwa saaana kwa vijana wake kuzamia Majuu wakiwa na afya njema kwa kazi za kubeba Maboxi!

    Bwana KAKA (BIG-Mwingereza) akaona aanzishe utaratibu huu ili Wabeba Mabox waje Wahudumie Wananchi wa Tanzania na Afrika!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 17, 2013

    NANI MJINGA ATAACHA KULIPWA POUND AKALIPWE SHILINGI?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 17, 2013

    Mdau wa Tisa (9)

    ''NANI MJINGA ATAACHA KULIPWA POUND AKALIPWE SHILINGI?''

    Hiyo kulipwa kwa POUND sio hoja, hoja ni wingi wa Fedha ikibadilishwa.

    HAO WALIOANZISHA MPANGO HUO WAMESHA FANYA UTAFITI HAJA KURUPUKA WAMEKUTA UBEBAJI WA MABOX MNALIPWA CHINI SANA HUKO (MAJUU), NIVILE TU MPO KWA WAZUNGU NDIO MNA BABAIKIA HICHO TU, HALAFU WAKAFANYA UFUATILIAJI WAKAKUTA PANA SEHEMU ZINGINE AFRIKA PANA VIPATO VYA JUU!

    KUANZISHWA KWA VITU KAMA HIVI KUNATANGULIWA NA UCHANGANUZI WA KITAALAMU KWANZA, WATU WAHAKURUPUKI.

    VITU KAMA:
    -FIELD STUDY
    -RESEARCH ANALYSIS
    -REPORT ANALYSIS
    -ECONOMIC ANALYSIS
    -LABOR ECONOMICS ANALYSIS

    Hebu angalia mfano Majuu unalipwa POUND 200 kwa Siku (NI SAWA NA TSH. 500,000/=) SASA INATOKEA KTK NCHI MOJAWAPO ZA AFRIKA (SIO TANZANIA PEKEE) UNAWEZA KUKUTWA UNALIPWA SANA NA TSHS.750,000/= KWA SIKU, MFANO ANGOLA,GHANA AU TUNISIA KWENYE SEKTA YA MAFUTA) SASA JE NI WAPI BORA UFANYE KAZI UINGERZAQ AU AFRIKA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...