Katika kuelekea kwenye mkutano wa tano wa kimataifa wa TICAD, watanzania wameshiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Watanzania wanashiriki kwenye matembezi hayo kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa ni wawakilishi pekee wa Bara Afrika kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, safari hii ikiwa ni matembezi ya 61.
Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sijaona amewashukuru Watanzania walioshiriki matembezi hayo, na kusema kwa njia hii pia, Watanzania tunatangaza utamaduni. Washiriki walivalia nguo za kiafrika.
Baadhi ya Watanzania waishio Japani wakiwa katika bustani ya Yamashita jiji Yokohama tayari kwa kushiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama.
mi nakwerwa sana na wawakilishi wetu wa Tanzania kuvaa nguo za kimasai kama watanzania wote ni wamasai- Mbona hamvai kanga basi japo mara moja
ReplyDeleteWamasai ni watu pia lakini statics haiwezekani ikachukuliwa kama ndio wengi wakati hata huko Arusha hawafikii asilimia ya wakaazi wengine
Tanzania hatuna vazi rasmi la kiutamaduni; tutake tusitake. Nikisema Tanzania namaanisha Bara na Visiwani ambako huko hawana mpango kabisaaaa na huo umasai mnaoubabaikia kuutangaza kama nembo ya taifa! na kama vazi hilo (la kimasai) linashobokewa kuwa vazi la kitaifa, basi hata Kenya, na hata Sudan nao inabidi wavae maana huko wapo kibao. Ni bora tubakie kuwa na bendera ya taifa tu, ambayo itaiwakilisha nchi.......FACT!
ReplyDeleteMdau hapo juu unashangaza sana! Umefikira kabla ya kuandika au umekurupuka? Hivi unataka uwakilishi wa mavazi equally kwenye nchi za watu, basi inawezekana waliovaa za kimasai wanatoka arusha! Wengine kama hawajataka kuvaa khanga unafanyaje? Swala la mavazi ni la mtu binafsi huwezi kumpangia,nyie ndio mnasababisha Tanzania isijulikane duniani! Mavazi ya kimasai yanavutia sana na ni unique! Mana kila kabila TZ lina vazi lake na hatuna vazi rasmi la nchi, fikiria kabla hujaandika. Hakuna aliyeuliza statistica inaonyesha wamasai wapo wangapi Arusha na ukiwa nje hakuna atakayekuuliza hivyo na ya nini yote hayo?
ReplyDeleteSasa, hebu nisaidie vazi gani jingine linao uwezo wa ku-distinguish Utanzania? Moreover Wamasai hawapo Tanzania? si Watanzania? Tungevaa ngu za wahehe unge lalamika pia, just stop being critical for the sake of it. Tafauta kuwa na hoja productive mpenzi!
ReplyDeleteNyie wote hapo juu nawashangaa sana. Mnaongelea vazi wakati kitu chenyewe ni shuka aina ya draft nyekundu.
ReplyDelete