Katika kuelekea kwenye mkutano wa tano wa kimataifa wa TICAD, watanzania wameshiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Watanzania wanashiriki kwenye matembezi hayo kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa ni wawakilishi pekee wa Bara Afrika kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka, safari hii ikiwa ni matembezi ya 61.

Balozi wa Tanzania nchini Japani Mh. Salome Sijaona amewashukuru Watanzania walioshiriki matembezi hayo, na kusema kwa njia hii pia, Watanzania tunatangaza utamaduni. Washiriki walivalia nguo za kiafrika.
Baadhi ya Watanzania waishio Japani wakiwa katika bustani ya Yamashita jiji Yokohama tayari kwa kushiriki kwenye matembezi ya hisani ya Yokohama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mi nakwerwa sana na wawakilishi wetu wa Tanzania kuvaa nguo za kimasai kama watanzania wote ni wamasai- Mbona hamvai kanga basi japo mara moja
    Wamasai ni watu pia lakini statics haiwezekani ikachukuliwa kama ndio wengi wakati hata huko Arusha hawafikii asilimia ya wakaazi wengine

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2013

    Tanzania hatuna vazi rasmi la kiutamaduni; tutake tusitake. Nikisema Tanzania namaanisha Bara na Visiwani ambako huko hawana mpango kabisaaaa na huo umasai mnaoubabaikia kuutangaza kama nembo ya taifa! na kama vazi hilo (la kimasai) linashobokewa kuwa vazi la kitaifa, basi hata Kenya, na hata Sudan nao inabidi wavae maana huko wapo kibao. Ni bora tubakie kuwa na bendera ya taifa tu, ambayo itaiwakilisha nchi.......FACT!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2013

    Mdau hapo juu unashangaza sana! Umefikira kabla ya kuandika au umekurupuka? Hivi unataka uwakilishi wa mavazi equally kwenye nchi za watu, basi inawezekana waliovaa za kimasai wanatoka arusha! Wengine kama hawajataka kuvaa khanga unafanyaje? Swala la mavazi ni la mtu binafsi huwezi kumpangia,nyie ndio mnasababisha Tanzania isijulikane duniani! Mavazi ya kimasai yanavutia sana na ni unique! Mana kila kabila TZ lina vazi lake na hatuna vazi rasmi la nchi, fikiria kabla hujaandika. Hakuna aliyeuliza statistica inaonyesha wamasai wapo wangapi Arusha na ukiwa nje hakuna atakayekuuliza hivyo na ya nini yote hayo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2013

    Sasa, hebu nisaidie vazi gani jingine linao uwezo wa ku-distinguish Utanzania? Moreover Wamasai hawapo Tanzania? si Watanzania? Tungevaa ngu za wahehe unge lalamika pia, just stop being critical for the sake of it. Tafauta kuwa na hoja productive mpenzi!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 04, 2013

    Nyie wote hapo juu nawashangaa sana. Mnaongelea vazi wakati kitu chenyewe ni shuka aina ya draft nyekundu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...