Rais Jakaya Kikwete (aliyenyoosha mkono) akitembelea Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere jijini Dares Salaam.kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa n Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Makazi(UNHABITANT) Phillemon Mutashubirwa kuhusu wanavyofanya kazi ya kusaidia watoto wa shule na wanawake kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere jijini Dares Salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akiangalia mafuta ya ubuyu na bidhaa zingine kwenye banda la Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF) kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu J. K Nyerere jijini Dares Salaam .Kutoka (kushoto) wa pili ni Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa (kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Stephen Emmanuel.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Du ulinzi kama obama.
ReplyDeleteHakuna kitu, wewe ulinzi wa Obama uliuona au ameusikia tu? Hapana chezeya marekani wewe!
ReplyDeleteWajasiliamali jamani jitahidini usafi, na uaminifu katika kutengeneza bidhaa hasa vya kula. Mafuta ya ubuyu ni mazuri kwa afya lakini wajanja wameanza kupaki korie kwenye chupa zenye lebo ya ubuyu.
ReplyDeletePia heshimuni na wale wanaowafadhili.
sabuni zinazotengenezwa na wajasiliamali zina kemikali inaathili ngozi. Yaani ukiogea ngozi inakuwa na mabaka kama fungasi
ReplyDeleteAu kuna kitu wanazidisha? hebu rekebisha kidogo tunazipenda.
Sabuni za ubuyu zina kiharufu fulani. Nadhani hicho wakitoe ndicho kinaleta madhara kwenye ngozi.
ReplyDeleteSi sabuni za ubuyu tu hata za mwarobaini n.k hebu rekebisheni kidogo.
Msijemkadhani zinapendwa . Ila mmoja akinunua harudi tena. Ili kuwa na bidhaa hii endelevu hebu angalia ni kuingo gani mle ndani ya sabuni kinaathili ngozi