Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abadalah Ulega akipata maelezo ya
ujenzi wa Mkuza wa bomba la gesi kutoka Mtwara kuelekea Dar es Salaam
toka kwa Eng Ahmeid Chinemba,Mratibu wa Mradi Mkoa wa Lindi alipokagua
kazi zinavyoendelea.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa,Abdalah Ulega akisikiliza maelezo toka
kwa Mratibu wa mradi huo,Eng Ahmeid Chinemba alipokuwa akikagua kazi
zinavyoendelea za kuandaa njia ya litakapopita Bomba la gesi kuanzia
vijiji vya somanga hadi Kiranjeranje wilayani Kilwa.
Kambi ya Njia nne wilayani Kilwa ni Moja kati ya kambi za Wachina Watakaoanza kutandaza bomba la kusafirisha Gesi kati ya Songosongo,Mtwara kuelekea Dar Zikiwa katika hatua ya umaliziaji wa majengo ya kuishi wafanyakazi..Kambi kama hii ipo katika kijiji cha Nangurukuru na Kitomanga wilayani Lindi.
Na Abdulaziz Video,Kilwa
Mkuu wa wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi,Abdallah Ulega amefanya ziara ya
siku moja kukagua maendeleo ya Ujenzi wa njia ya bomba la
gesi(Mkuza)kazi ambayo imeanza kati ya Songosongo,Mtwara Dar na
kutarajiwa kazi zote kukamilika ndani ya Miezi 18.
Ulega alitembelea kati ya kijiji cha Somanga na Kiranjeranje kukagua
kazi inavyoendelea na changamoto za na kuzungumza na wananchi na
kuwataka waitumie vyema fursa hiyo katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni
pamoja na kutoa Ushirikiano kwa wawekezaji ili wanufaike na huduma za
kimaendeleo katika wilaya yetu.
“Ndg zangu wana kilwa hizi fursa mzitumie kwa kusomesha watoto wenu
ili wanufaike na ajira za gesi hii,Hata hivyo nasikitika kwa kuwa
nimeambiwa na hawa wachina kuwa mmeanza kuwaibia jamani tutafika
mlikuwa kwa amani na hawa wageni mnapata ajira za muda mnalipwa sasa
angalieni tumewaletea askari nyie wenyewe mnaona raha?Serikali
imejipanga na kusimamia mnanufaika na miradi hii…alimalizia Ulega
alipokuwa akisalimiana na wananchi wa njia nne wilayani Kilwa.
Kwa Upande wake mratibu wa Mradi huo wa Mkuza Mkoa wa Lindi,Eng Ahmeid
Chinemba akitoa maelezo ya kazi hizo kwa Mkuu wa wilaya
huyo,Alibainisha kuwa kazi hiyo ambayo Itagharimu Jumla ya Dola Bilion
1.2 inatekelezwa na kampuni ya mabomba ya petrol ya China imeanza kwa
kuandaa mkuza kati ya Songosongo Nyamwage kuelekea Dar es salaam na
Somanga Nangurukuru Mtwara.
Chinemba pia alieleza kuwa sambamba na ukamilishaji wa mkuza huo pia
tayari kambi kuu 3 za za malazi na ofisi kwa wafanyakazi wa kazi hizo
zipo katika hatua ya mwisho katika Vijiji vya Njianne,Nangurukuru na
Kitomanga ambapo pia mabomba ya kazi yakiwa yanapokelewa katika kambi
ya Kiranjeranje.
Kufuatia Uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilayani Kilwa na
kusafirishwa kwenda Dar tayari inauzwa kwa zaidi ya Viwanda 30,huku
jamii ya wakazi kijiji cha Songosongo wakinufaika na utumiaji wa
nishati ya umeme bila malipo huku Halmashauri ya wilaya Kilwa
ikikusanya kodi ya Huduma pamoja kusaidia huduma mbalimbali za kijamii


Uncle naomba uniulozie kwa viongozi wetu inakuaje miradi ya kichina inaajiri wachina kibao kwa hata zile kazi zinazoweza lufanywa na watanzania miradi kama hii si ndio fursa ya watz kukuza kipato chao ?
ReplyDeleteJibu la mdau hapo juu:Kawaida wachina ndivyo wafanyavyo ktk makubaliano yao na hilo halina ujanja kwa viongozi wetu wa afrika nzima si tu tanzania.Kwa sasa china imejaa watu wasio na ajira na seriakli yao inajitahidi kuwapa nafasi nyingi za nje ili wachina watoke nchini na kwenda kufanya kazi nje ya china,matokeo yake ndio hayo tunayoyaona sasa hapa nyumbani.Uhalisia ni kwamba mpaka afrika magharibi kilio ni hikohiko, wanakaba sehemu zote mpaka ufagizi.
ReplyDelete