
Inaelezwa kuwa Sheikh Ponda, ambaye naye alikuwa mmoja wa watoa mada, aliondoka baada ya kongamano kumalizika akiwa katika gari ndogo kabla ya kupatwa na mkasa huo.
Inaelezwa kuwa baada ya kujeruhiwa Sheikh Ponda alikimbizwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu, ambako inasemekana hakukaa sana kwani alitoweka na jina lake halikuwahi kuandikikao wa kwenye daftari la wagonjwa wafikao hospitali.
Hadi sasa habari za uhakika kuwa amejeruhiwa kiasi gani na nani aliyemjeruhi hazijapatikana. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amekanusha madai hayo ya kupigwa risasi kwa Sheikh Ponda na kueleza kuwa hali ni shwari mkoani Morogoro kwa sasa baada ya machafuko ya muda mfupi mida ya jioni ya leo.
Kamanda Shilogile amesema kuwa yeye hajui hali yake maana polisi walizuia gari lake ili wamkamate kwa tuhuma za uchochezi zinazomkabili, lakini wananchi wakaanza kuwashambulia polisi na wakafanikiwa kumtorosha kupitia mlango wa uwani wa hospitali ya mkoa.
Amesema baada ya shambulio hilo, Polisi walilazimika kurusha risasi hewani kuwatawanya wananchi. Kamnada Shilogile anatoa wito kwa mtu yeyote anayejua alipo Ponda awaarifu polisi mapema
Msimuua Shehe ponda mtasababisha fujo katika nchi, badala yake mpeni fomu za kugombea urais mwaka 2015.
ReplyDeletemaisha tz yamekuwa ni uonevu kila siku si uchumi wala dini, wapeleke upuuzi wao somalia au mali waone, hawatasahau kama walivyofunzwa sudan.
ReplyDeletemichuzi tafuta habari kamili wacha uzugani, Ponda amepigwa risasi uwanjani.
ReplyDeleteHizi habari zikowazi na hali yake nimbaya sana.
Ponda ndiye nani nchii hii Bwana? Ukitaka kuwasambaratisha kondoo muueni mchungaji! Mkamateni huyo mtoto wa ibilisi huyo
ReplyDeleteMimi nadhani watu kama sheikh ponda wanatakiwa kuzuiwa kwa gharama yoyote ile ,ili wasiendelee kuleta uchochezi usio na faida yoyote nchi hii .kila mwenye shida ya kumjua mungu asome vitabu vyake na si kuwapigia watu kelele nani yuko sahihi na nani anakosea ,these people serve their ego, it just make them feel better to tell people that others are wrong and they are right,simply they are sick people and dangerous people .
ReplyDeletekaka hapo juu sudan na mali inahusu nini tanzania 0 nchi yetu ni ya amani ukiwa raia mwema hupati tatizo, ukikosea hata shule au kazini utachukuliwa hatua
ReplyDeleteChondechonde msimuue shehe Ponda nasisitiza tena chondechonde, mtasababisha vurugu nchi nzima.mkamateni akiwa hai mwekeni kizuizini.
ReplyDeletemimi Xvery komba -Mbinga.
haipendezi mtu kutoa maoni ya ajabu ajabu hasa kwa jambo linaowahusu kundi au jamii ambyo si yako.kumbuka kuwa poda ni kiongozi wa waislamu na hivyo uapokosa la kuchagia acha wenye jambo lao waoyeshe wanavyoguswa.
ReplyDeletesome people are possessed with demon, to couse corruption, destroy, and killing
ReplyDelete