Taarifa ambazo bado kuthibitishwa kutoka Morogoro zinadai  kwamba Sheikh Issa Ponda (pichani) amejeruhiwa na kile kinachosadikwia kuwa ni risasi akitoka  kuhudhuria kongamano la kidini lililofanyika mjini humo na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali.

Inaelezwa kuwa Sheikh Ponda, ambaye naye alikuwa mmoja wa watoa mada, aliondoka baada ya kongamano kumalizika akiwa katika gari ndogo kabla ya kupatwa na mkasa huo.
Inaelezwa kuwa baada ya kujeruhiwa Sheikh Ponda alikimbizwa hospitali ya mkoa kwa ajili ya matibabu, ambako inasemekana hakukaa sana kwani alitoweka na jina lake halikuwahi kuandikikao wa kwenye daftari la wagonjwa wafikao hospitali.
Hadi sasa habari za uhakika kuwa amejeruhiwa kiasi gani na nani aliyemjeruhi  hazijapatikana. Kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa  Morogoro,  Faustine Shilogile, amekanusha  madai  hayo  ya  kupigwa  risasi  kwa Sheikh Ponda  na  kueleza  kuwa  hali  ni  shwari  mkoani  Morogoro    kwa  sasa  baada  ya  machafuko  ya  muda  mfupi  mida  ya  jioni ya leo.
Kamanda Shilogile  amesema  kuwa  yeye  hajui hali yake maana polisi walizuia gari lake  ili wamkamate  kwa  tuhuma  za  uchochezi  zinazomkabili, lakini wananchi wakaanza kuwashambulia polisi   na  wakafanikiwa  kumtorosha kupitia mlango wa uwani wa hospitali ya mkoa.
Amesema baada  ya  shambulio hilo, Polisi  walilazimika  kurusha risasi hewani kuwatawanya wananchi. Kamnada Shilogile anatoa  wito  kwa  mtu  yeyote  anayejua  alipo  Ponda awaarifu  polisi  mapema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Msimuua Shehe ponda mtasababisha fujo katika nchi, badala yake mpeni fomu za kugombea urais mwaka 2015.

    ReplyDelete
  2. maisha tz yamekuwa ni uonevu kila siku si uchumi wala dini, wapeleke upuuzi wao somalia au mali waone, hawatasahau kama walivyofunzwa sudan.

    ReplyDelete
  3. michuzi tafuta habari kamili wacha uzugani, Ponda amepigwa risasi uwanjani.
    Hizi habari zikowazi na hali yake nimbaya sana.

    ReplyDelete
  4. Ponda ndiye nani nchii hii Bwana? Ukitaka kuwasambaratisha kondoo muueni mchungaji! Mkamateni huyo mtoto wa ibilisi huyo

    ReplyDelete
  5. Mimi nadhani watu kama sheikh ponda wanatakiwa kuzuiwa kwa gharama yoyote ile ,ili wasiendelee kuleta uchochezi usio na faida yoyote nchi hii .kila mwenye shida ya kumjua mungu asome vitabu vyake na si kuwapigia watu kelele nani yuko sahihi na nani anakosea ,these people serve their ego, it just make them feel better to tell people that others are wrong and they are right,simply they are sick people and dangerous people .

    ReplyDelete
  6. kaka hapo juu sudan na mali inahusu nini tanzania 0 nchi yetu ni ya amani ukiwa raia mwema hupati tatizo, ukikosea hata shule au kazini utachukuliwa hatua

    ReplyDelete
  7. Chondechonde msimuue shehe Ponda nasisitiza tena chondechonde, mtasababisha vurugu nchi nzima.mkamateni akiwa hai mwekeni kizuizini.

    mimi Xvery komba -Mbinga.

    ReplyDelete
  8. haipendezi mtu kutoa maoni ya ajabu ajabu hasa kwa jambo linaowahusu kundi au jamii ambyo si yako.kumbuka kuwa poda ni kiongozi wa waislamu na hivyo uapokosa la kuchagia acha wenye jambo lao waoyeshe wanavyoguswa.

    ReplyDelete
  9. some people are possessed with demon, to couse corruption, destroy, and killing

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...