THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji
Mstaafu, Mheshimiwa Damian Z. Lubuva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mjumbe wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wakili wa Kujitegemea, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Hillary
Mkate kilichotokea nyumbani kwake Kinondoni Jijini Dar es Salaam tarehe 1
Novemba, 2013.
“Nimeshtushwa,
nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Jaji
Mstaafu, Mheshimiwa Hillary Mkate ambaye amewahi kuitumikia Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kwa uadilifu mkubwa, na hivyo kutoa mchango stahiki katika
kuiongoza Tume hiyo kufanya kazi zake kikamilifu”,
amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
Rais
Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Jaji Hillary Mkate, enzi za uhai wake, kama
kiongozi mwadilifu na mchapakazi hodari ambaye alitumia vipaji vyake vyote alivyojaaliwa
na Mwenyezi Mungu kutoa haki kwa wananchi mbalimbali waliokuwa wakizitafuta
haki zao kutokana na sababu mbalimbali.
“Kutokana
na msiba huu mkubwa, Ninakutumia wewe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Damian Lubuva, Watumishi wote wa Mahakama na Wanasheria kote
nchini kwa kuondokewa na mwenzao, Jaji Mstaafu na Wakili wa Kujitegemea, Mheshimiwa
Hillary Mkate. Namuomba Mwenyezi Mungu,
Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Amina”,
ameongeza kusema Rais Kikwete.
Aidha
Rais Kikwete amemuomba Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Damian Lubuva kumfikishia
Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa Familia ya Marehemu Jaji Mstaafu,
Hillary Mkate kwa kupotelewa na Kiongozi na Mhimili wa Familia.
Amewahakikishia
Wanafamilia hao kuwa yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo
ya mpendwa wao. Amewaomba wawe na moyo
wa uvumilivu, utulivu na subira katika kuomboleza msiba huu kwa vile yote ni Mapenzi
yake Mola.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4
Novemba, 2013
Libina mkatte pole sana na msiba
ReplyDelete