THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Damian Z. Lubuva kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wakili wa Kujitegemea, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Hillary Mkate kilichotokea nyumbani kwake Kinondoni Jijini Dar es Salaam tarehe 1 Novemba, 2013.

“Nimeshtushwa, nimesikitishwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa za kifo cha Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Hillary Mkate ambaye amewahi kuitumikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa uadilifu mkubwa, na hivyo kutoa mchango stahiki katika kuiongoza Tume hiyo kufanya kazi zake kikamilifu”, amesema kwa masikitiko Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.

Rais Kikwete amesema alimfahamu Marehemu Jaji Hillary Mkate, enzi za uhai wake, kama kiongozi mwadilifu na mchapakazi hodari ambaye alitumia vipaji vyake vyote alivyojaaliwa na Mwenyezi Mungu kutoa haki kwa wananchi mbalimbali waliokuwa wakizitafuta haki zao kutokana na sababu mbalimbali.

“Kutokana na msiba huu mkubwa, Ninakutumia wewe Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Damian Lubuva,  Watumishi wote wa Mahakama na Wanasheria kote nchini kwa kuondokewa na mwenzao, Jaji Mstaafu na Wakili wa Kujitegemea, Mheshimiwa Hillary Mkate.  Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza Mahala Pema Peponi Roho ya Marehemu, Amina”, ameongeza kusema Rais Kikwete.

Aidha Rais Kikwete amemuomba Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Damian Lubuva kumfikishia Salamu zake za Rambirambi na pole nyingi kwa Familia ya Marehemu Jaji Mstaafu, Hillary Mkate kwa kupotelewa na Kiongozi na Mhimili wa Familia.

Amewahakikishia Wanafamilia hao kuwa yuko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya mpendwa wao.  Amewaomba wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na subira katika kuomboleza msiba huu kwa vile yote ni Mapenzi yake Mola.  

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Novemba, 2013





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Libina mkatte pole sana na msiba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...